Featured Kitaifa

MRADI WA LTIP KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI HALMASHAURI YA MUFINDI

Written by mzalendoeditor

 

Katibu Tawala wa halmashauri ya Mufindi Bw.Frank Sichalwe,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau kujadili rasimu ya Mpango wa matumizi ya ardhi uliondaliwa na mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi (LTIP) kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo.

 

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Katibu Tawala wa halmashauri ya Mufindi Bw.Frank Sichalwe,wakati akifungua Mkutano wa wadau kujadili rasimu ya Mpango wa matumizi ya ardhi uliondaliwa na mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi (LTIP) kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo.

Na.Alex Sonna-MUFINDI

WATENDAJI  wa vijiji, mitaa, madiwani pamoja na watendaji wengine wa halmshauri ya Mufindi wametakiwa kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi unaosimamiwa  na mradi wa usalama wa milki za ardhi (LTIP) ili uwe na tija kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo Julai 22,2023 na Katibu Tawala wa halmashauri ya Mufindi Bw.Frank Sichalwe,wakati akifungua Mkutano wa wadau kujadili rasimu ya Mpango wa matumizi ya ardhi uliondaliwa na mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi (LTIP) kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo.

Amesema kuwa mradi huo una lengo la kumaliza migogoro ya matumizi ya ardhi na migogoro ya mipaka ya vijiji na kutumika kama dira ya matumizi sahihi ya kila kipande cha ardhi ndani ya Halmashauri ya Mufindi.

“Halmashauri yetu inawategemea sana kusaidia mradi huu kuwa na manufaa nyinyi ndiye ambao mpo huko kwa wananchi mnajua ni kwa namna gani migogoro ya ardhi ilivyokuwa ni kero kwa wananchi wenu lazima mhakikishe kuwa mpango wa matumizi ya ardhi unasaidia kuondoa migogoro ili kupata mradi mwingine na kumaliza vijiji vitakavyo bakia”amesema Bw.Sichalwe,

Hata hivyo wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusaini mkataba wa mkopo wa zaidi ya Sh. bilioni 340 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili kupanga matuzi bora ya ardhi katika halmasahuri mbalimbali nchini.

Sichalwe, amesema halamashauri hiyo inamshukuru Rais Samia kwa kuridhia kusaini mkataba huo wa mkopo ambao unakwenda kuwezesha kutatuliwa kwa migogoro ya ardhi na mipaka ya vijiji katika maeneo mbalimbali nchini.

“Mradi huu utasaidia kupanga matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogo ya ardhi isiyokuwa ya lazima kama jana tulikuwa eneo moja kuna migogoro ya ardhi kupita kiasi tunashukuru sana Rais kwa mkopo huu wa benki ya dunia”amesema Sichalwe

Kwa upande wake  Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi  Mradi  Bi.Tumaini Setumbi,amesema katika mradi huu tumeweza kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi katika wilaya sita ikiwemo wilaya ya Mufindi ni mmoja wapo maandalizi ya mpango huu itaweza kusaidia kuepusha migogoro mbalimbali inayoweza kujitokeza kwenye Jamii.

”Katika uandaaji wa matumizi haya ya ardhi ya wilaya Mradi umeweza kuhusisha jamii mbalimbali wameweza kushirika katika maandaliza haya kwa kutumia madodoso mbalimbali yakuweza kuonyesha maenoe mbalimbali yaliyopo katika wilaya hiyo”

Naye Diwani wa kata ya Igomabavanu Veronica Kilungumtwa, amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuwezesha mradi huo ambao unakwenda kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi nchini.

“Mpango wa matumizi bora ya ardhi unakwenda kuwa shirikishi hivyo utasaidia kuondoa migogoro ya ardhi iliyopo lakini pia kusaidia watu kupata hati milki ambazo watazitumia kupata mikopo katika taasisi za kifedha”amesema 

About the author

mzalendoeditor