Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO LA MIONZI HOSPITALI YA RUFAA RUVUMA

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alilozindua  akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo tarehe 22 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa wataalamu wa Afya wakati akikagua vifaa tiba vilivyopo katika Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alipowasili kuzindua jengo hilo akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo tarehe 22 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akieleza juu ya Mashine ya X- Ray ya Kisasa iliopo katika Hospitali ya Ruvaa ya Mkoa wa Ruvuma wakati akikagua vifaa tiba vilivyopo katika Jengo la Mionzi la Hospitali hiyo alipowasili kuzindua jengo hilo akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo tarehe 22 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alilozindua  akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo tarehe 22 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akivuta kitambaa kuweka jiwe la msingi la Uzinduzi wa Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alilozindua akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo tarehe 22 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wananchi mbalimbali wa Kijiji cha Mwengemshindo mara baada ya kuzindua Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma alilozindua  akiwa ziarani mkoani Ruvuma leo tarehe 22 Julai 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wahudumu wa afya kwa kuhakikisha inaboresha Maisha yao na vitendea kazi.

Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 22 Julai 2023 wakati akizindua Jengo la Mionzi la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Ametoa wito kwa watoa huduma za afya kutunza vifaa tiba ikiwemo kuweka utaratibu mzuri wa matengenezo ili viweze kutoa huduma kwa wananchi wakati wote.

Makamu wa Rais amesema ni dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha inasogeza huduma bora za afya karibu na wananchi ikiwemo kupeleka vifaa tiba vya kisasa katika hospitali za mikoa ili kuwapunguzia gharama wananchi kufuata huduma hiyo maeneo ya mbali.

Aidha Makamu wa Rais amesema Serikali inathamini mchango wa watoa huduma za afya kwa kuwa wanamchango mkubwa katika kuwahudumia wananchi na kuokoa Maisha yao. Amewasihi wahudumu wa afya kuendelea kuwahudumia wananchi kwa upendo mkubwa.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Ruvuma yenye lengo la Kusikiliza changamoto za wananchi, kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo

About the author

mzalendoeditor