Featured Kitaifa

CWT YATOA MSAADA YA MITUNGI YA GESI KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KISHAPU

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Mkude akikabidhi jiko la gesi kwa mwakilishi kutoka shule ya Igaga Sekondari
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Mkude akikabidhi jiko la gesi kwa mwakilishi wa shule
Mitungi161 iliyotolewa na Chama Cha Walimu CWT wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwenye shule za msingi na Sekondari wilayani Kishapu pamoja sukari kwa lengo la kuongeza ufaulu mashuleni na kuondokana na uharibifu wa mazingira.
Mitungi161 iliyotolewa na Chama Cha Walimu CWT wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwenye shule za msingi na Sekondari wilayani Kishapu pamoja sukari kwa lengo la kuongeza ufaulu mashuleni na kuondokana na uharibifu wa mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Mkude akizungumza wakati wa kugawa majiko hayo kwa Walimu Huku akiwasisitiza wakawe mabalozi wa matumizi ya nishati hiyo ili kuweka mazingira salama kutokana na watu kukata miti hovyo.
Katibu wa mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga bw. Godfrey Mbussa akizungumza kwenye hafla ya ugawaji majiko ya gesi yaliyotolewa na CWT Kishapu.
Katibu wa Chama Cha Walimu CWT mkoa wa Shinyanga Mwl Allen Kizito akizungumza kwenye hafla ya ugawaji majiko ya Gesi wilayani Kishapu na kusema kuwa CWT ipo kwa dhumuni la kuwatetea walimu na kupeleka hoja za kwa serikali kwa ajili ya kuwaboreshea maslahi na miundombinu ya kazi zao.
Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT) mkoa wa Shinyanga Mwl.Allen Kuzito akizungumza kwenye hafla ya ugawaji majiko ya gesi yaliyotolewa na Chama Cha Walimu CWT wilayani Kishapu.
Wawakilishi wa shule za msingi na Sekondari wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Joseph Mkude kabla ya zoezi la ugawaji majiko ya gesi na sukari kutoka Chama Cha Walimu CWT wilaya ya Kishapu.
Mwalimu wa shule ya msingi Mwabusiga iliyoko wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na mhasibu wa CWT Wilayani humo Mwl.Goerge Gailanga akizungumza baada ya kupokea jiko la gesi kutoka CWT Kishapu.
Mwalimu Queen Wa shule ya msingi Mwangongo baada ya hafla ya ugawaji majiko ya gesi
Katibu wa Chama Cha Walimu CWT wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mwl. Luhende Lyongoma akizungumza baada ya hafla ya ugawaji majiko ya gesi
Mwalimu Joseph Mangw’ena wa shule ya Sekondari isoso wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akizungumza baada ya hafla ya ugawaji majiko ya gesi
 
 
Na Sumai Salum – Kishapu
 
Chama Cha Walimu (CWT) wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kimetoa msaada wa mitungi 161 ya gesi yenye thamani ya shilingi ya shilingi Milioni 7.2 kwenye shule zote za msingi na sekondari wilayani humo ikiwa ni sehemu ya motisha  kwa walimu na uhamasishaji utunzaji mazingira wilayani humo.
 
 
Hafla fupi ya makabidhiano ya mitungi hiyo ya gesi imefanyika leo Julai 20,2023 kwenye viwanja vya ofisi za CWT zilizoko Mhunze wilayani Kishapu.
 
 
Katibu wa CWT Wilaya ya Kishapu Mwl. Luhende Lyongoma amesema lengo utoaji wa mitungi kwa kila shule ni kuwapa motisha walimu ili wapate muda mwingi wa kuwa shuleni na kuwafundisha wanafunzi kwa makini ili waongeze ufaulu kwa Wilaya.
 
 
“Tunatambua hii ni sekta nyeti ambayo imebeba dhamana ya wataalamu mbalimbali kwenye taifa na ulimwengu huu hivyo walimu wanapokuwa kwenye maeneo yao ya kazi watakuwa wakiandaa wenyewe kifungua kinywa na pia ikiwezekana kuandaa chakula ambapo serikali kupitia halmashauri yetu sikivu tunashauri kuwa ni vema pia kama likitengwa fungu kwa ajili ya kuwajazia gesi pindi inapoisha”, ameongeza Mwl. Lyongoma.
 
 
 
 
Akizungumza kwenye hafla hiyo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude licha ya kuwapongeza kwa jambo zuri walilolifanya amesema kuwa msaada huo utaendana na dhima ya serikali ya awamu ya sita ya utunzaji wa mazingira ambapo sasa nishati hiyo nzuri na itasaidia utunzaji wa mazingira kwa kutokata miti hovyo.
 
 
“Kwa kweli hatujuwahi kusikia wala kufikiria kama CWT inaweza kufanya jambo kubwa kama hili, kwa sababu walimu ni kioo cha jamii hivyo muende kuwa mabalozi wa matumizi ya nishati ya gasi na si kuni wala mkaa. Kama tunavyojua Wilaya yetu hii miti inatumia muda mrefu kukua na kwa gharama kubwa hivyo wanafunzi, wazazi na walezi wakiona kwanza nyie mnatumia gesi itakuwa chachu ya wao na familia zao kuiga mfano huu mzuri na tukafikia mahali serikali inataka tufike”, amesema Mkude.
 
 
Mkude ameleleza kuwa serikali inayonia njema kwenye sekta ya elimu ndiyo maana hadi sasa wilaya imepokea fedha kutoka serikali kuu na tayari imejenga katika kijiji cha Mwamala kilichopo kata ya Itilima nyumba ya walimu mbili kwa moja (2) na kiasi cha sh. Milioni 600 za ujenzi wa shule Mwaweja na nyumba za walimu.
 
 
 
 
Kwa upande wake Katibu wa mbunge wa Jimbo la Kishapu Bw. Godfrey Mbussa amesema walimu wanayo nafasi kubwa ya mchango wa maendeleo kwa taifa na ofIsi ya mbunge inao wajibu wa kuishauri serikali kuhusu mapungufu na uhitaji wa walimu kwani walimu wakinyong’onyea taaluma itashuka hivyo amewashauri kuwa ofisi ya mbunge ipo kwa ajili yao.
 
 
Nao baadhi ya Walimu kutoka shule mbalimbali wamesema kuwa nishati hiyo itawasaidia kuokoa muda kwani shule nyingi zipo mbali na maeneo ya kupata chakula hivyo hutumia muda mrefu kutembea wakitafuta chakula jambo ambalo limekuwa likiwafanya kupoteza muda mwingi na kutotimiza majukumu yao ya ufundiahaji kwa weledi.
 
 
“Yaani hii itatusaidia sana sisi tulioko vijijini kwa sababu tutapata chakula kwa uhakika kabisa kwani tutaandaa wenyewe kulikoni unaweza kutoka kwenda migahawani kula kisha baada ya hapo unaanza kusikia vibaya hali ya afya ya tumbo na kushindwa kutimiza wajibu na pia itasaidia kuongeza tija ya ufundishaji na kuongeza ufaulu” amesema Mwl. George Gailanga mwalimu wa Mwabusiga shule msingi.

About the author

mzalendoeditor