Burudani Featured

NCHI ZAIDI YA 20 ZASHIRIKI TAMASHA LA ZIFF MJINI ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma akifunga Tamasha la 26 la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) Julai 02, 2023 mjini Zanzibar.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma akikabidhi tuzo ya filamu bora na ndefu ya kisayansi (Sci-Fi) ya EONII wakati wa kufunga Tamasha la 26 la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) Julai 02, 2023 mjini Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akikabidhi tuzo ya filamu kwa mmoja wa washindi wa tuzo hizo wa Tanzania wakati wa kufunga Tamasha la 26 la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) Julai 02, 2023 mjini Zanzibar.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla ya kufunga Tamasha la 26 la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) Julai 02, 2023 mjini Zanzibar.

Na Eleuteri Mangi, WUSM, Zanzibar

Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) limehitimishwa ambapo nchi zaidi ya 20 zimeshiriki ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Cameroon, Qatar, Congo DRC, Misri, Algeria, Tunisia, Morocco, Italy, Israel, Ufaransa, Uingereza, Ireland, Afghanistan, Denmark, Hispania, Angola, Namibia, Afrika Kusini, China, Zambia, Zimbabwe na Uswizi.

Tamasha hilo limehitimishwa Julai 2, 2023 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma ambaye alitoa tuzo kwa filamu bora na ndefu ya kisayansi (Sci-Fi) ya EONII iliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salaam

Tamasha hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Dkt. Kilonzo Kiagho ni miongoni mwa wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani kutoka mataifa hayo.

Ni mwaka wa 26 tangu Tamasha la ZIFF lilipoanzishwa mwaka wa 1997 kuendeleza na kukuza tasnia ya filamu na mambo mengine ya kiutamaduni kama kichocheo cha ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa kikanda.

About the author

mzalendoeditor