Featured Michezo

MICHEZO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA USHIRIKA YAFANA 

Written by mzalendoeditor

 

Mwenyekiti wa Kamati  ndogo ya Michezo,Burudani na Matangazo ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya ushirika Duniani,Bw.Ibrahim Kadudu,akizungumza wakati wa Michezo ya Soka,Netiboli, kuvuta kamba na kukimbiza Kuku michezo hiyo ikijumuisha wachezaji kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Sheila la Ukaguzi la Vyama vya Ushirika (COASCO) na Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU) lililofanyika  katika uwanja wa Chuo cha  Uhazini mkoani Tabora kuelekea  maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani Julai Mosi mwaka huu.

Na.Alex Sonna-TABORA

KUELEKEA Maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani Julai mosi mwaka 2023 kumefanyika michezo mbalimbali katika Viwanja vya Chuo cha Utumishi wa Umma.

Michezo ambayo imepigwa  ni soka,netiboli kuvuta kamba na kukimbiza Kuku ikiwakutanisha  wafanyakazi na watumishi wa ushirika na Shirikisho la vyama vya Ushirika.

Mwenyekiti wa Kamati ya ndogo ya Michezo,Burudani na Matangazo ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya ushirika Duniani,Ibrahim Kadudu  amesema michezo hiyo ilifanyika katika uwanja wa Chuo cha  Uhazini mkoani Tabora.

Amesema timu zilizoshiriki michezo hiyo ikijumuisha wachezaji kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Sheila la Ukaguzi la Vyama vya Ushirika (COASCO) na Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU).

Amesema michezo hiyo  ni maalum kwa ajili ya  kuadhimisha siku ya ushirika inayotarajiwa kufanyika Julai mosi mwaka huu.

“Ushirika asili yake ni mashirikino na  michezo yote asili yake ni mashirikino hakuna mchezo ambao unaweza kuchezwa na mtu mmoja inachezwa na zaidi ya moja,”amesema Mwenyekiti huyo.

Amesema faida zinazopatikana ni pamoja na  mahusiano na uchumi kwa watu mbalimbali.

“Niwasisitize wanaushirika michezo ni  eneo la muhimu kuimarisha afya na watumishi tuendelee kufanya mazoezi hata baada ya bonanza hili,”amesema Bw.Kadudu

Pia ametoa rai kwa wachezaji iwe chachu kuendeleza kile ambacho wamekianzisha  ili kuimarisha  afya.

Pamoja na mambo mengine washindi walioibuka kukimbia kwenye gunia no Issa Ahamed na Agustino Abdul Karim kutoka TCDC, kukimbia kuku Issa ameendelea kubaki mshindi akifuatiwa na Raphael. Nae Adolf Ndunguru akifuatiwa na Noel Steven washindi kipindi cha pili wakitokea TCDC.

Aidha, mchezo wa mpora wa Pete Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) ilishambulia magoli 30 dhidi ya TCDC Kwa goli 10. Mgeni Rasmi Mrajis Msaidizi wa Geita Doreen Mwanri ametoa zawadi ya mipira Kwa timu za Netiboli kuunga mkono juhudi za wanamichezo.

Wachezaji wa Timu za Mpira wa Pete wakichuano vikali ambapo Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kimeibuka na ushindi wa kishindo wa magoli 30-10  dhidi ya TCDC mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chuo cha  Uhazini mkoani Tabora kuelekea  maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani Julai Mosi mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati  ndogo ya Michezo,Burudani na Matangazo ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya ushirika Duniani,Bw.Ibrahim Kadudu,akizungumza wakati wa Michezo ya Soka,Netiboli, kuvuta kamba na kukimbiza Kuku michezo hiyo ikijumuisha wachezaji kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Sheila la Ukaguzi la Vyama vya Ushirika (COASCO) na Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU) lililofanyika  katika uwanja wa Chuo cha  Uhazini mkoani Tabora kuelekea  maadhimisho ya  siku ya Ushirika Duniani Julai Mosi mwaka huu.

Mgeni Rasmi Mrajis Msaidizi wa Geita Doreen Mwanri akitoa  zawadi ya mipira Kwa timu za Netiboli kuunga mkono juhudi za wanamichezo.

About the author

mzalendoeditor