Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS KUZINDUA MAONYESHO YA KILELE YA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JKT

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Mpango kesho Julai mosi, 2023 anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi wa maonyesho ya shughuli za uzalishaji mali na huduma zinazotolewa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 60 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo.

Akizungumza Jijini Dodoma mara baada ya kukagua maandalizi ya maonyesho hayo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa ambapo amewataka wakazi wa Dodoma na viunga vyake kukaribia katika maonyesho hayo yatakayoanza kesh

“Niwakaribishe watu wote waweze kushiriki nasi katika maonyesho haya, ambayo yatafanyika kila siku mara yatakapozinduliwa na Dkt Mpango hadi Julai 9, 2023,” amesema

Amesema kilele cha maadhimisho hayo ya JKT kitakuwa Julai 10, 2023 ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa JKT, Meja Jenerali, Rajabu Mabele amesema kuanzia kesho wanaanza wiki ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

“Yapo maonyesho mbalimbali ya bidhaa zinazozalishwa na vikosi vyetu vya Jeshi la Kujenga Taifa lakini zipo shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni zetu zitakuwa zinaonyeshwa hapa,” amesema.

Amesema kuna bidhaa zitakazokuwa zikiuzwa katika maonyesho hayo na nyingine wateja wanaweza kutoa oda ya kuzalishiwa.

Meja Jenerali Mabele amesema pia katika maonyesho wananchi watapata nafasi ya kuelimishwa shughuli zinazofanywa na JKT ikiwemo ufagaji na uvuvi.

Pia amesema wameweka eneo la kuonyesha ni jinsi gani wanawasaidia vijana na vitu gani wanapata katika jeshi hilo kama sehemu ya shamba darasa.

Aidha, amesema kutakuwepo wanyama wa pori, vikundi na burudani mbalimbali zikiwemo bendi za jeshi hilo.

About the author

mzalendoeditor