Featured Kitaifa

JESHI LA POLISI LAKARIBISHWA KUTUMIA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUBAINI UHALIFU

Written by mzalendoeditor

 

Kaimu Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete akifungua kikao cha siku Moja ya utekelezaji wa makubaliano ya kujengeana uwezo na Jeshi la Polisi.

Kamishina wa Jeshi la Polisi kitengo cha Uchunguzi wa Kimtandao Bw Shabani Hiki akielezea umuhimu wa Sayansi na Teknolojia katika kubaini wahalifu.

Na.Mwandishi Wetu

Kaimu Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete ametoa wito kwa Jeshi la Polisi nchini kutumia Sayansi na Teknolojia kubaini wahalifu.

Aliyasema hayo tarehe 21 Juni, 2023 wakati akifungua kikao cha kwanza cha utekelezaji wa mkataba wa makubaliano uliosainiwa baina ya taasisi hizo  tarehe 31 Agosti ,2022 kwa lengo la kujengeana uwezo katika kutatua changamoto za kiuchunguzi kubaini wahalifu.

 Profesa  Mshandete alitoa wito kwa watumishi wa Jeshi la polisi nchini kupata ujuzi wa muda mfupi au mafunzo ya kisayansi na teknolojia kutoka katika taasisi hiyo  yatakayowawezesha kuwabaini wahalifu.

Kwa Upande wake  Mkuu wa shule ya Sayansi ya Mawasiliano ya Komputa na Uhandisi Dkt Mussa Ali alisema, utekelezaji wa makubaliano ya kujengeana uwezo  ,timu za utafiti kutoja  shule ya Sayansi ya Mawasiliano ya Komputa na Uhandisi na Shule ya Biashara na Ubinadamu zinaifanyia kazi.

Naye Kamishina wa Jeshi la polisi Bw. Shabani Hiki alieleza  jinsi maabara za Jeshi la Polisi zinazofanya kazi zao za kiuchunguzi kwa kutumia  ya sayansi na teknolojia .

Aliongeza kuwa  utumiaji wa Sayansi na teknolojia utasaidia upatikanaji wa matokeo chanya katika tafiti kuepuka kesi nyingi kurudishwa mahakamani kutokana ukosefu wa taarifa sahihi za mwalifu.

About the author

mzalendoeditor