Featured Kitaifa

KATAMBI AWAAPA MAAGIZO MAZITO WAKURUGENZI PSSSF NA NSSF

Written by mzalendoeditor

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Patrobas Katambi, ameagiza, akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 20,2023 jijini Dodoma kuhusu changamoto wanazokutana nazo baadhi ya wanachma na wastaafu wanapofuatailia mafao kwenye mifuko ya Pesheni.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Patrobas Katambi, ameagiza wakurugenzi wakuu wa mifuko ya pensheni ya PSSSF na NSSF kuhakikisha waajiri wote wanalipa na kuwasilisha madeni ya michango ya watumishi wao kila mwezi ili kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wastaafu nchini.

Katambi, amesema hayo leo Juni 20,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto wanazokutana nazo baadhi ya wanachma na wastaafu wanapofuatailia mafao kwenye mifuko ya pesheni.

“Nafahamu pamekuwepo na changamoto kwa baadhi ya waajiri kutowasilisha michango au kuwasilisha michango pungufu ya watumishi wao pamoja na kuvunja sheria kutowasilisha michango ni usumbufu kwa wastaafu”amesema Mhe.Katambi

Katambia amesema kutokana na hali hiyo anaagiza mameneja wote wa mikoa wasikilize na kutoa elimu kuhusu taarifa za wanachama kuhusu michango na mafao.

“Kuhakikisha waajiri wote wanalipa na kuwasailisha madeni ya michanago ya watumishi wao kila mwezi, kila meneja wa mkoa awasilishe majina ya waajiri sugu wanaodaiwa michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku saba kuanzia leo”amesema Mhe.Katambi

Pia amesema kila mfuko uhakikishe mwanachama analipwa ndani ya siku 60 za kisheria kwa wanachama wote ambao nyaraka zao zimewasilishwa kwenye mfuko kwa ukamilifu.

Aidha, ameagiza waajiri wote wanawasilisha taarifa za kustaafu kwa mtumishi wake miezi sita kabala ya kustaafu ili kupunguza ucheleweshaji.

“Kutokuwasailisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ni kosa kisheria, michango iwasailishwe kwenye mifuko bila shuruti, waajiri wasiotoa mikataba kwa wafanyakazi wao ni kinyume na sheria ya ajira na mahusianao kazini Na. 6 ya mwaka 2004”amesema

About the author

mzalendoeditor