Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA KIWANDA CHA A TO Z KWA KUZINGATIA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Written by mzalendoeditor

 

Na Mwandishi wetu, Arusha

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imekipongeza kiwanda cha A to Z Textills Mills kwa kuzingatia sheria za afya na usalama mahali pa kazi.

Hayo yamebainishwa  na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Fatma Toufiq walipotembelea kiwanda hicho kwa ajili kukagua masuala ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema kiwanda hicho kina wafanyakazi 8000 na asilimia 70 ya wafanyakazi hao ni wanawake ambao wamepewa mikataba ya kazi na kujumuishwa katika mifuko hifadhi ya jamii (PSSSF) na kuchangia asilimia 0.5 kwenye mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF).

Ametoa wito kwa waajiri na wawekezaji kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na sheria za kazi ili kutengeneza ajira na kulipa kodi bila shuruti.

About the author

mzalendoeditor