Featured Kitaifa

KONGAMANO LA METROLOJIA AFRIKA MASHARIKI KUJADILI VIPIMO SEKTA YA AFYA

Written by mzalendoeditor
SERIKALI kuendelea kufanya uwekezaji katika uboreshaji wa Vipimo hususani katika sekta ya afya kwa kuhakikisha kuwa vipimo vinakidhi ubora wa kimataifa na hatimaye kuchagiza ustawi biashara.
 
Akizungumza leo Juni 19,2023 pindi akimwakilisha Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashantu Kijaji Kwenye Kongamano la Metrolojia la afrika Mashariki Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema katika kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara nchini ni vyema kuboresha Sekta ya afya ili kutoa fursa kwa wananchi kuwa na afya njema itakayowawezesha kujikita katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
 
Amesema Rais Samia anafanya kazi kubwa kuifungua nchi kiuchumi ambapo ameweka mazingira bora na wezeshi ya ufanyaji biashara.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dk.Athuman Ngenya amesema kongamano hilo lenye Kauli mbiu isemayo “Metrolojia katika afya” limelenga kutambua umuhimu wa vipimo katika sekta ya afya na linajikita katika kutoa elimu kwa wadau muhimu katika sekta ya afya na kusaidia kuboresha vipimo vinavyotumika katika taasisi mbalimbali za afya nchini
 
Naye Afisa Viwango Mwandamizi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Ramadhani Mfaume ameweka wazi kuwa kongamano la mwaka huu limejumuisha nchi saba a Afrika Mashariki kwa lengo la kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali za vipimo katika nchi hizo huku Mwenyekiti wa uratibu wa Kongamano hilo kutoka shirika la Viwango nchini Kenya Mhandisi Josephat Bangi akibainisha kuwa pamoja na mambo mengine kongamano hilo litasaidia kuwa na vipimo vyenye ubora sawa katika nchi za afrika mashariki

About the author

mzalendoeditor