Featured Kitaifa

TAMISEMI KUWACHUKULIA HATUA WATAKAOKWAMISHA JITIHADA ZA RAIS SAMIA KWENYE UJENZI WA SHULE ZA MSINGI

Written by mzalendoeditor

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa maelekezo kwa viongozi na watendaji Manispaa ya Singida wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa ujenzi wa shule za msingi na ukarabati wa madarasa kupitia mradi wa boost unaosimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Baadhi ya wananchi Wilayani Singida wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa ujenzi wa shule za msingi na ukarabati wa madarasa kupitia mradi wa boost unaosimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi akielekea kukagua utekelezaji wa ujenzi wa moja ya shule za msingi katika Manispaa ya Singida. Aliombatana nao ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi na watendaji wa wilaya hiyo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa kwenye ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi wa moja ya shule za msingi katika Manispaa ya Singida. Aliombatana nao ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi na watendaji wa Serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akitoa taarifa utekelezaji wa ujenzi wa moja ya shule za msingi katika Manispaa ya Singida kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa ujenzi wa shule za msingi na ukarabati wa madarasa katika Manispaa hiyo.

Mwonekano wa moja ya darasa katika Manispaa ya Singida lililo katika hatua za mwisho za ujenzi wake.

Mafundi wakiendelea kujenga madarasa katika moja ya shule iliyopo Manispaa ya Singida.

Na. James K. Mwanamyoto-Ofisi ya Rais TAMISEMI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi amesema ofisi yake haitosita kumchukulia hatua atakayebainika kukwamisha ujenzi wa shule za msingi na ukarabati wa madarasa kwani fedha za ujenzi na ukarabati huo zimetolewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuboresha miundombinu ya elimu msingi.

Mhe. Ndejembi ametoa rai hiyo mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kikazi katika Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Singida iliyolenga kukagua utekelezaji wa ujenzi wa shule za msingi na ukarabati wa madarasa kupitia mradi wa boost unaosimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Mhe. Ndejembi amesema kuwa, watakaobainika kukwamisha mradi huo watachukuliwa hatua kali ili iwe ni fundisho kwa wengine wenye nia ovu ya kukwamisha miradi yenye tija kwa wananchi na maendeleo ya taifa. 

Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati miradi yote ya ujenzi wa shule na na ukarabati wa madarasa ili thamani ya fedha ionekane. 

“Ninawaomba msimuangushe Mhe. Rais, hakikisheni mnakamilisha ujenzi ifikapo tarehe 30 Juni, 2023 kama ilivyopangwa ili kumpa nguvu Mhe Rais ya kuleta fedha nyingine,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Mhe. Ndejembi amefafanua kuwa, Mhe. Rais ametoa bilioni 230 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule za msingi pamoja na ujenzi wa shule mpya kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa nchini, kitendo ambacho kinaonesha dhamira yake njema ya kuhakikisha watoto wanapata elimu katika mazingira bora.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya yake shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi wilayani kwake.

Mheshimiwa Ndejembi amehitimisha ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida kwa kuwasisitiza Wakurugenzi Wote nchini na Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari kuhakikisha wananunua vifaa vyote vya ujenzi vinavyohitajika kabla ya mwaka wa fedha kuisha ili miradi inayoendelea kutekelezwa iweze kukamilika kwa wakati.

About the author

mzalendoeditor