Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa kitaifa wa kupitia na kurasimisha Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto awamu ya pili (MTAKUWWA II) Jijini Dodoma Juni 14, 2023
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya sera na Mipango kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na Makundi Maalum Sifuni Msangi akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa kitaifa wa kupitia na kurasimisha Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto awamu ya pili (MTAKUWWA II) Jijini Dodoma Juni 14, 2023
Baadhi ya washiriki kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali wakifuatilia Mkutano wa kitaifa wa kupitia na kurasimisha Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto awamu ya pili (MTAKUWWA II) Jijini Dodoma Juni 14, 2023.
Mwakilishi kutoka shirika la Wanawake wa Umoja wa Mataifa ( UN WOMEN) Bi. Maya Hansen akitoa salamu za wadau wakati mkutano wa kitaifa wa kupitia na kurasimisha Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto awamu ya pili (MTAKUWWA II) Jijini Dodoma Juni 14, 2023
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju akia katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa kitaifa wa kupitia na kurasimisha Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto awamu ya pili (MTAKUWWA II) Jijini Dodoma Juni 14, 2023
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM
Na WMJJWM, DODOMA
Serikali imesema itahakikisha awamu ya pili ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II) 2023/24-2027/28) inaimarisha Uchumi wa Kaya kwa kuweka Mazingira Salama na wezeshi ikiwemo usimamizi na utekelezaji wa sheria kwenye Maeneo ya Umma na Mitandaoni ili kutokomeza Ukatili.
Hayo yamebainika wakati wa kikaokazi kilicho ongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amoni Mpanju kwenye Mapitio ya (MTAKUWWA II 2023/24-2027/28) kilichofanyika Juni 14, 2023 jijini Dodoma.
Mpanju amesema suala la uimarishwaji wa Uchumi wa kaya ni miongoni mwa Maeneo nane (8) ambayo yatakwenda kuguswa Mpanju wakati wa awamu pili ya ya mpango kazi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA II 2023/24-2027/28)
“Nimejulishwa kuwa Rasimu ya Mpango kazi huu imekamilika na imeandaliwa kulingana na matokeo ya tathmini iliyofanyika na kuja na maeneo nane (8) ambayo ni Kuimarisha Uchumi wa Kaya; Mila na desturi; Mazingira Salama katika Maeneo ya Umma na Mitandaoni; Malezi, Msaada wa Familia na Mahusiano; Utekelezaji na Usimamizi wa Sheria, Utoaji Huduma kwa Manusura wa Vitendo vya Ukatili; Mazingira Salama Shuleni, Nyumba Salama na Stadi za Maisha pamoja na Uratibu, Ufuatiliaji na Tathmini. Maeneo haya yamewekwa mahsusi kabisa kwa ajili ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto” amesema Mpanju.
Wakili Mpanju ameongeza kuwa asasi za kiraia, vingozi wa Dini, Wazee wa Kimila na Vyombo vya Habari wamekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha usawa wa jinsia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Shukrani za dhati kwa Wadau wote kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na kuhakikisha makundi yote ndani ya jamii yanalindwa dhidi ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto,” Aliongeza Mpanju.
Kwa Upande wake Mwakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Stela Sasita amesema TAMISEMI itahakikisha inaupa kipaumbele utekelezaji wa mpango huo kwenye maeneo wanayoyasimamia hususani ni ngazi za Mikoa na Halmashauri
“Kama ambavyo mnajua kwamba, sisi TAMISEMI tunaratibu shughuli ngazi ya Halmashauri na ngazi za mikoa ambapo wako wananchi na jamii nzima huko kwahiyo sisi tutakuwa watekelezaji wakubwa wa mpango huu ” amesema Stella
Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya waziri mkuu Bw. Said Mabie amesema kuwa, ofisi yao inatekeleza sera ya kinga ya jamii ambayo inahusika na ulinzi wa jamii katika Nyanja zote.
Akiongea wakati wa kikao hicho Muwakilishi kutoka ICS Bw. Sokoine Kudeli amesema asasi za kiraia nchini bado zitaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha watoto pamoja na akina mama wanakua kwenye mazingira Salama.