Featured Michezo

YANGA BINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO AZAM

Written by mzalendoeditor
ULIKUWA Msimu bora sana kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Timu ya Yanga mara baada ya kutwaa taji la kombe la Shirikisho Azam (ASFC) kwa kuwachapa bao 1-0 Matajiri wa Chamazi  Azam Fc Mchezo wa Fainali uliopigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
 
Yanga waliingia uwanjani wakiwa na nyota wake watatu muhimu kutokuwepo Mfugaji wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika  Fiston Kalala Mayele,Stephane Aziz Ki ambao wameitwa kwenye timu zao za taifa huku Jesus Moloko akitumikia Kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya Mbeya City.
 
Shujaa wa Yanga Sc ni Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Kenned Musonda alifunga kwa kichwa dakika ya 13 , bao ambalo limedumu mpaka dakika 90 ya mchezo.
 
Yanga Sc imefanikiwa kuchukua taji hili mara mbili mfululizo na kuendelea kujiwekea rekodi muhimu katika msimu huu ambao wameweza kuvaa medali nne ikiwemo medali,Kombe la Ngao ya Jamii, kombe la Shirikisho barani Afrika baada kushika nafasi ya pili,Kombe la NBC Ligi na Kombe la ASFC.

About the author

mzalendoeditor