Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuzindua Kongamano la Kitaifa la Kujengewa Uelewa Juu ya Athari za Sauti Zilizozidi Viwango katika Nyumba za Ibada, Juni 12, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuzindua Kongamano la Kitaifa la Kujengewa Uelewa Juu ya Athari za Sauti Zilizozidi Viwango katika Nyumba za Ibada, Juni 12, 2023. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Kongamano la Kitaifa la Kujengewa Uelewa Juu ya Athari za Sauti Zilizozidi Viwango katika Nyumba za Ibada, Juni 12, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Kujengewa Uelewa Juu ya Athari za Sauti Zilizozidi Viwango katika Nyumba za Ibada baada ya kuzindua kongamano hilo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Juni 12, 2023.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa maelekezo nane ikiwemo Halmashauri kutenga maeneo ya kujenga nyumba za ibada ili kupunguza malalamiko miongoni mwa jamii.
Majaliwa ameyasema hayo Jana Jijini dar es salaam wakati alipokuwa akifungua kongamano la kitaifa la kujenga uelewa juu ya athari za sauti zilizozidi viwago katika nyumba za ibada lililoshirikisha viongozi wa dini na kimila.
Mei 6 mwaka huu akiwa jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa alitaka shughuli za dini kuendelea kama kawaida na kutoa maelekezo kwa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania (JMAT) kwa kushurikiana na Baraza la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) kukutana na kuratibu suala hilo.
Amesema Serikali itaendelea kushauriana na Jumuiya ya Maridhiano katika kuona namna bora ya kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia mahitaji ya jamii na kulinda afya za Watanzania.
Amesema kila dhehebu lina muda wa msingi wa dua au sala, lakini upo muda wa ziada na kuwataka viongozi wa dini kukaa na kuangalia kama muda wa ziada unatakiwa kuongezewa nguvu ya ziada.
“Ili kupunguza malalamiko miongoni mwa jamii kila Halmashauri inapaswa kutenga maeneo kwaajili ya ujenzi wa nyumba za ibada pamoja na kufuata mipango miji,”amesema Majaliwa.
Amesema mipango ya ujenzi wa nyumba za ibada unapaswa kuanza pale taasisi inaposajiliwa kwa kufuata mipango ya matumizi bora ya ardhi na sio kusubiri mtu ajenge kisha baadae kuja kubomolewa, suala hilo sio sawa.
Pia kwa watoaji wa vibali wametakiwa kufanya ufuatliaji wa mara kwa mara, ili kujiridhisha maelekezo yaliyotolewa ndio yanayofuatwa ikiwa ni be pamoja na miongo ya Nemc.
“Kwa wakuu wa mikoa, wekeni utaratibu wa kukutana na na viongozi wa taasisi mara kwa mara mkitoa elimu lakini fanyeni tathinini ya majengo yanayotoa kelele zilizozidi na kutoa muda wa kufunga vifaa vya kudhibiti kelele”,amesema Majaliwa
Akizungumzia suala la sheria Majaliwa aliwataka viongozi wa dini kukaa na kuangalia, endapo inawakandamiza wawe huru kusema kwa kuwa Serikali inaheshimu dini zote.
“Kitu chochote kisipokuwa na utaratibu kina kero, fanyeni mapitio ya kelelele za ziada suala lolote likiwekewa utaratibu sio kero,” amesema Majaliwa
“Unakuta kuna sheria zimewekwa lakini utekelezaji wake una changamoto, pitieni sheria na kanuni zake jama kuna mapungufu ua kuna sehemu haiko sawa wasilisheni Serikalini iliniweze kufanyiwa kazi,”amesema Majaliwa
Akizungumza katika kongamano Mkurugenzi Mkuu wa Nemc Dk Samweli Gwamaka alisema kuanzia Januari hadi Mei wamepokea zaidi ya taarifa 500 za kelele zinazotokana na nyumba za ibada.
Amesema kufuatia taarifa hizo Serikali imeandaa muongozo na kutoa maelekezo mahususi katiaka makundi mbalimbali, ikiwemo wanaozalisha sauti zinazozidi viwango kwenye nyumba za ibada.
“Zauti zilizozdi viwango zimeleta athari kubwa kwa jamii, ikiwemo waumini kutosiskia vizuri, kuathiri shughuli za uzalishaji kiuchumi lakini pia wapo watu wenye matataizo mbalimbali ikiwemo wagonjw,”amesema Dk Gwamaka.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo alisema wanamshukuru Waziri Mkuu kwa sababu kupitia taarifa iliyotolewa na NEMC walipokea takwimu takribani 521 ambazo zimeonesha wazi kuwa tatizo la sauti zilizozidi viwango ni kubwa nchini. Up
Amesema wamekutana katika kongamano hilo kwa lengo la kupeana maelekezo ya kutosha katika upande wa kanuni na sheria za mazingira na kuangalia namna bora na nzuri ya kufanya biashara na ibada ziendelee lakini zikifuata taratibu na sheria za nchi.
“Sisi siku zote tutakuwa tayari kuhakikisha maelekezo yote ya serikali yanafanyiwa kazi, lakini kuangalia namna bora zaidi kupitia taasisi yetu ya NEMC kufanikisha kila jambo linakwenda kama lilivyopangwa,” amesema Jafo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya maridhiano ,Sheikh Alhad Mussa Salum alisema keleke sio uchafuzi wa mazingira kelele ni sauti zilizozidi.
Amesema Mwenyezi Mungu ana haki zake na waja wake nao wana haki zao, dhumuni la Kongamano hilo ni kuangalia ni kwa namna gani ya kukaa pamoja na kuweka suala hilo kwenye mazingira mazuri.
Mei 8 mwaka huu NEMC ilutangaza kuzzifungia jumla ya baa na kumbi za starehe 89 zimefungiwa baada ya kubaini kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango vinavyotakiwa.