Featured Kitaifa

WAZIRI NDALICHAKO ATETA NA MENEJIMENTI YA OFISI YAKE

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiongoza kikao cha majadiliano alipokutana na menejimenti ya ofisi yake katika jengo la OSHA leo tarehe 7 Juni, 2023 jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa menejimenti wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akichangia wakati wa kikao hicho kilichofanyika jengo la OSHA leo tarehe 7 Juni, 2023 jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Leonard Mchau (aliyesimama) akieleza jambo wakati wa kikao hicho.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi wakipitia kitabu cha Mpango wa Taifa kwa Watu wenye Ualbino 2023/2024 – 2027/2028.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

……..

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Ofisi hiyo leo tarehe 7 Juni, 2023 katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.

Lengo la kikao hicho ni kufanya majadiliano kuhusu maendeleo ya ukarabati wa Vyuo vinne (4) vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu, hatua iliyofikiwa ujenzi wa Vyuo vitatu (3) vya Watu wenye Ulemavu, Mpango wa Taifa wa Watu wenye Ualbino na Madeni ya Waajiri ambao hawajawasilisha michango kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Prof. Ndalichako pia amewataka viongozi hao kuendelea kuchapa kazi kwa weledi na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ili kufikia azma ya Serikali na wananchi wanaowahudumia.

Vile vile, Mhe. Ndalichako amesisitiza menejimenti hiyo kuendelea kutangaza mafanikio na mambo makubwa yanayofanywa na serikali kwa maslahi ya taifa.

About the author

mzalendoeditor