Featured Kitaifa

PROF.NOMBO AISHUKURU SERIKALI YA CHINA KWA MSAADA WA VITABU

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo ameishukuru Serikali ya China kwa juhudi inazoonesha katika kuhakikisha somo la lugha ya Kichina linafundishwa kwa ufasaha nchini.

Profesa Nombo ametoa shukrani hizo jijini Dar es Salaam wakati akipokea msaada wa vitabu 2,700 kutoka nchini China kwa lengo la kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kichina.

Amesema ufundishaji wa lugha ya kichina kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne hapa nchini umeendelea kuimarika tangu kuanzizshwa kwake mwaka 2016.

“Kwa sasa ziko shule za Serikali 18 zinazofundisha lugha ya kichina, Shule mbili ambayo ni Morogoro na Usagara zimechukua hatua zaidi na kufundisha lugha hiyo kwa wanafunzi wa kidato cha tano wanaochukua mchepuo wa Kiswahili, kingereza na lugha ya kichina (KEC),”amesema Profesa Nombo.

Profesa Nombo ameongeza kwa sasa wizara ipo kwenye mapitio ya Sera na mabadiliko ya mitaala na moja ya mapendekezo yaliyopo ni kufundisha lugha mbalimbali ambapo wachina wameanza.

“Nimeelezwa kuwa mwezi Aprili 2023 mligawa vitabu 2,304 na leo vitabu 2,700 na kufanya idadi ya vitabu mlivyotoa kuwa 5004 hii itasidia katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kichina na kuleta uwiano mzuri wa vitabu kwa wanafunzi ,”amesema Profesa Nombo

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania CHEN Mingjian amesema urafiki wa Tanzania na China ni wa muda mrefu na kwamba wanaendelea kuufurahia.

Amesema anaamini siku zote maarifa yana nguvu, hivyo vitabu vilivyogawiwa vitasaidia walimu na wanafunzi kujifunza lugha ya Kichina kwa ufasaha ikiwa ni pamoja na kuielewa historia ya nchi ya China na utamaduni wao.

About the author

mzalendoeditor