Hacklink panel

Hacklink Panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Backlink paketleri

Hacklink Panel

Hacklink

Hacklink

Hacklink

Hacklink

Hacklink

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink satın al

Hacklink satın al

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Illuminati

Hacklink

Hacklink Panel

Hacklink

Hacklink Panel

Hacklink

Masal oku

Hacklink Panel

Hacklink Panel

Hacklink panel

Masal Oku

Hacklink

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink Panel

Hacklink

Hacklink

Hacklink

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink

Hacklink

Buy Hacklink

Hacklink

Hacklink

Hacklink satın al

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Hacklink panel

Masal Oku

Hacklink panel

Hacklink satın al

Hacklink Panel

https://www.newstrendline.com/bilgi-kutusu/

Hacklink Panel

Hacklink Panel

Hacklink Panel

Hacklink Panel

Hacklink Panel

Hacklink Panel

Hacklink Panel

Hacklink Panel

Hacking forum

Hacklink panel

sakarya escort bayan

Samsun Avukat

dedektör

vdcasino giriş

holiganbet

betsalvador

mavibet

mavibet giriş

jojobet

bets10 sorunsuz

grandpashabet güncel giriş

https://www.newstrendline.com/

palacebet

ultrabet giriş

lunabet

mavibet

setrabet

jojobet giriş

betebet

gonebet

jojobet

jojobet

holiganbet

mavibet

marsbahis

kingroyal

bets10

bets10 giriş

vdcasino giriş

millibahis

vipslot

festwin

parmabet

celtabet

kulisbet giriş

mavibet

holiganbet güncel giriş

mavibet giriş

piabellacasino giriş

piabellacasino

artemisbet giriş

mavibet

mavibet giriş

piabellacasino

piabellacasino giriş

piabellacasino

deneme bonusları veren siteler

deneme bonusu veren siteler

marsbahis giriş

festwin

doeda

av ซับไทย

vdcasino

xxxเย็ดยับ

jojobet güncel giriş

jojobet güncel giriş

casibom güncel giriş

casibom giriş

casibom

grandpashabet giriş

cratosroyalbet, cratosroyalbet giriş

deneme bonusu

deneme bonusu

sahabet

portobet

dinamobet giriş

casibom

casibom

casibom

casibom

jojobet

casibom

casibom

casibom

casibom

casibom

Hacklink panel

betturkey

betnano

test55

Hacklink panel

Hacklink giriş

casibom giriş

jojobet

jojobet

jojobet

jojobet

padişahbet

marsbahis

kralbet giriş

casibom

casibom

betsin

meritking

marsbahis

deneme bonusu

betsa

meritking

crypto scam

meritking

meritking

madridbet

meritking

deneme bonusu

spyhackerz

jojobet

uyuşturucu satın al

jojobet güncel giriş

İmajbet

royalbet

imajbet

betgross

biabet

artemisbet giriş

casibom

deneme bonusu

casibom giriş

deneme bonusu veren siteler

deneme bonusu veren siteler

deneme bonusu veren siteler

deneme bonusu veren siteler

deneme bonusu veren siteler

pokerklas

perabet

betsat

bets10

vdcasino

jojobet

Jojobet

matbet

redwin

deneme bonusu

deneme bonusu

vdcasino

1xbet

starzbet

giftcardmall/mygift

kulisbet

holiganbet giriş

holiganbet

grandpashabet

girne escort

magusa escort

dedebet

holiganbet

tubidy

kralbet

Girne Escort

deneme bonusu

deneme bonusu

deneme bonusu

deneme bonusu

Featured Kitaifa

UKWELI KUHUSU MGOMO WA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO

Written by Alex Sonna
 
Wafanyabiashara wakubwa wakwepa kodi tangu enzi za Awamu ya Nne watajwa kuwa chanzo cha mgomo
 
Maamuzi ya Rais Samia ya kutuma timu ya mawaziri Kariakoo yazima mgogoro
 
Kamati ya watu 14 kutoka Serikalini, wafanyabiashara yapewa jukumu la kumaliza mzizi wa fitna
 
***
IMEBAINIKA kuwa wafanyabiashara wakubwa wanaokwepa kodi za forodha za kuingiza makontena ya bidhaa kutoka China na baadhi ya wanasiasa ndiyo waliokuwa chanzo kikuu cha mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo, huku wafanyabiashara wadogo wakitumika kama chambo na vipaza sauti kuchochea mgomo huo.
 
Wafanyabiashara hao ambao wanaagiza mzigo mkubwa wa bidhaa kutoka China, Uturuki, Dubai na nchi nyingine huku wakikwepa kodi wakati wanaingiza makontena yao ya bidhaa kwenye Bandari ya Dar es Salaam, wamewachochea wafanyabiashara wadogo wa Kariakoo kugoma ili kushinika Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) isiwabane kwenye ukwepaji wao wa kodi.
 
Baadhi ya wanasiasa nao wameshiriki kuchochea mgomo huo kwa maslahi yao binafsi ya pesa na kisiasa.
 
Hivi karibuni umetokea mgomo wa wafanyabiashara kwenye soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, ambalo ndiyo soko kuu la bidhaa mbalimbali za jumla na rejareja zinazouzwa nchini na hata kwenye baadhi ya nchi jirani.
 
Mgogoro huo ulisababisha Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kutuma timu ya viongozi waandamizi, ikiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba, na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Ashatu Kijaji.
 
Baada ya kikao cha wazi cha mawaziri na wafanyabiashara, Serikali iliunda kamati ya watu 14, ikijumuisha maafisa waandamizi wa serikali na wafanyabiashara ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa malalamiko ya wafanyabiashara wa Kariakoo.
 
Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya soko la Kariakoo zimethibitisha kuwa wafanyabiashara wadogo wametumika kushiriki kwenye mgomo huo na wafanyabiashara wakubwa wanaoingiza makontena ya bidhaa kutoka China na nchi nyingine ili kutengeneza mgogoro wa kisiasa.
 
“Kuna wafanyabiashara wanajulikana tangu enzi za Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete ambao walikuwa ni vinara wa kukwepa kodi kwa kuingiza makontena ya bidhaa kutoka China, Dubai, Uturuki na nchi nyingine ndiyo chanzo cha mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
 
“Wafanyabiashara hao vinara wa kukwepa kodi wamebanwa na TRA kwenye Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia, hadi makusanyo ya kodi yamevunja rekodi kwa kufikia wastani wa Shilingi trilioni 2 kwa mwezi ambayo haijawahi kutokea tangu tupate uhuru.”
 
Baada ya kuona kuwa wamebanwa na TRA, hususan kwenye eneo la kudhibiti utozaji kodi wa makontena ya bidhaa kutoka China, na jitihada za kudhibiti maghala ya bidhaa kwenye maduka Kariakoo, wafanyabiashara hao wakubwa wakawachochea wafanyabiashara wadogo wa Kariakoo waanzishe mgomo wao uliodumu kwa siku kadhaa.
 
“Kusema ukweli TRA imefanya kazi nzuri ya kuwabana wakwepaji kodi hawa wakubwa kwa kutaka kila kontena la mizigo linaloingia nchini lilipiwe kodi stahiki. Hizi vurugu zote tunazoona Kariakoo ni matokeo ya hawa wafanyabiashara wakubwa wakwepaji kodi kutaka kuzua taharuki ili TRA iache kuwabana,” alisema mfanyabiashara mmoja wa Kariakoo.
 
Baadhi ya matatizo waliyolalamikia wafanyabiashara ni utitiri wa kodi na tozo za Serikali kuu na Serikali za Mitaa, viwango vikubwa vya kodi ya TRA, rushwa miongoni mwa baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu wa umma wa TRA, TANROADS, LATRA na Polisi.
 
“Baadhi ya malalamiko ya wafanyabiashara wa Kariakoo, ikiwemo kuombwa rushwa na watumishi wachache wa TRA wasiokuwa na maadili, viwango vikubwa vya kodi na utitiri wa tozo za Serikali za Mitaa yana hoja. Lakini nyuma ya pazia waliochochoea mgomo huo ni hao wafanyabiashara wakubwa wanaoingiza makontena ya bidhaa kutoka China na nchi nyingine,” alisema.
 
Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonesha kuwa kwa mwaka 2021 peke yake, Tanzania iliingiza bidhaa zenye thamani ya karibu dola za Marekani Bilioni 2.7 kutoka China, ambayo ni sawa na Shilingi trilioni 6.5, huku sehemu kubwa ya mizigo hiyo kutoka China ikiwa ni bidhaa zinazouzwa kwenye soko la Kariakoo.
 
“Lengo la wafanyabiashara wakubwa hawa ambao ni vinara wa kukwepa kodi ni kuchochea mgomo wa wafanyabiashara wadogo wa Kariakoo ili kuishinikiza Serikali iwaagize TRA waache kuwabana wakwepa kodi hawa kwenye mamia ya makontena ya bidhaa kutoka nje ambayo wanaingiza kila mwezi na kwenye maghala yao ambayo wanayatumia kukwepa kodi,” alisema muuza duka mmoja wa Kariakoo.
 
“Tunaipongeza Serikali ya Rais Samia kwa kusikiliza kilio cha wafanyabiashara wadogo wa Kariakoo kuhusu ukubwa wa viwango vya kodi na utitiri wa tozo kutoka manispaa, lakini tunaomba Serikali iwe makini na hawa wafanyabiashawa wakubwa wakwepa kodi wanaotaka kututumia wafanyabiashara wadogo kufanikisha ukwepaji wao wa kodi.”  

 

About the author

Alex Sonna