Featured Kitaifa

SPIKA DKT.TULIA AIPONGEZA TTCL KWA UTENDAJI KAZI WAKE

Written by mzalendoeditor

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua mabanda mbalimbali katika Maonesho yanayoendelea  viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Mei 18,2023.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson,akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),Mhandisi Peter Ulanga wakati alipotembelea banda la Shirika hilo katika Maonesho yanayoendelea  viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Mei 18,2023.Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Mathew Kundo.

Meneja Biashara  TTCL Dodoma Bi.Leyla Pongwe,akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la shirika hilo kwa niaba ya  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),Mhandisi Peter Ulanga wakati  katika Maonesho yanayoendelea  viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Mei 18,2023.

Na.Bolgas Odilo-DODOMA

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Tulia Ackson amelipongeza  Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kufanya vizuri katika utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na  kufikisha huduma za mawasiliano ya intaneti kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Pongezi hizo amezitoa leo Mei 18,2023 wakati alipotembelea banda la Shirika hilo katika Maonesho yanayoendelea  viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Spika Tulia amesema ameoneshwa  mambo mengi katika banda la TTCL   lakini suala  la mkongo kufika nyumbani  ni jambo la muhimu   kwani matumizi ya data na teknolojia ni muhimu.

“Nitume nafasi hii kuwapongeza  TTCL kwa kutuleta huduma hii naamini zitapunguza gharama ya matumizi ya bando ambayo  tumekuwa tunalalamika.

“Tumeona mmefika Kilimanjaro,hiyo itakuwa nzuri kwa sababu kutakuwa  hakuna uongo uongo,piga tujue umefika kileleni  kama mmefika pale ni vizuri nawaongeza sana mnafanya kazi nzuri,”amesema Spika Tulia.

Kuhusu zoezi la anuani za makazi,Spika Tulia amesema : “Nimefurahi kuona zoezi hili la anuani ya makazi ambalo limeanza mapema mwaka jana na sasa tumefikia sehemu yule ambaye amesajiliwa anuani  yake anaweza kupata huduma  kwa kutumia simu yoyote,”.

Kwa upande wake Meneja Biashara  TTCL Dodoma Bi.Leyla Pongwe amesema wamefika bungeni kuwaonesha  wabunge mikakati ambayo wanayo katika kuisaidia serikali kwenye kuchagiza kufikia uchumi wa kidigital mpaka mwaka 2025.

Amesema wanajivunia kwa sasa kwani wameweza kufikisha huduma ya intaneti katika mlima Kilimanjaro.

“Zamani ilikuwa mtalii akipanda  juu anakuwa hapatikanai ila sasa hivi mtalii anapatikana.Sasa hivi tunamletea mtanzania fiber mpaka nyumbani kwake analipia kifurushi kwa mwezi kwani ili  kufikia uchumi wa kati lazima uwe na intaneti,”amesema meneja huyo.

Amesema wamewaonesha wabunge ukiwa na intaneti Fiber  ya TTCL unaweza kuwasaliana hata ukiwa mbali mradi  una intaneti  popote ulipo  na unawea kufanya kwa kupitia application  ya simu.

Amesema wameweza kufikisha  mkongo wa Taifa  mpaka katika maeneo ya mipakani mwa  Tanzania na sasa hivi wanaanza  kutoka nje ili kufikisha mawasiliano katika Nchi zote za jirani

“Tunakituo cha data centre ambacho kinatumika kutunza taarifa  na data za watoa huduma na serikali tunawaribisha watu wote kutunza kumbukumbu zao,”amesema 

About the author

mzalendoeditor