Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Patrobas Katambi (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Sightsavers wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi kwa Watu wenye Ulemavu unaotekelezwa na Shirika la Sightsavers kwa wanufaika 360 uliofanyika leo Mei 18,2023 Jijini Dar es Salaam
NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu,Kazi,Vijana,ajira na watu wenye ulemavu Patrobas Katambi amewataka Mashirikisho ya watu wenye ulemavu kuwa na chama kimoja ili kuweze kupaza sauti serikali iweze kuwasaidia kwa umoja wao kuliko kujigawa kwa makundi kutokana na utofauti wa ulemavu walionao.
Akizungumza na Wanahabari Leo Mei 18,2023. Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe.Patrobas Katambi wakati akizundua Mradi wa uwezeshaji kiuchumi kwa watu wenye ulemavu unaotekelezwa na Shirika la Sightsavers kwa wanufaika 360 amesema kupitia bilioni 1 iliyotengwa na taasisi hiyo kwa lengo la kuwasaidia na kuwajengea uwezo walemavu katika kujikwamua kiuchumi na kuweza kufanya miradi mbalimbali kwa ufanisi zaidi serikali itaendelea kuwashika mkono taasisi zenye nia ya dhati na Maendeleo kwa taifa la Tanzania.
Aidha Katambi amesema Serikali itaendelea kulinda haki na stahiki za watu wenye ulemavu kwa kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kubadilisha mitazamo hasi kuwa chanya kuhusu watu wenye ulemavu.
Pia amewataka watu wasio na ulemavu kuzingatia sheria na kulinda haki za watu wenye ulemavu na kubainisha kuwa serikali inatarajia kufanya mabadiliko ya sera ya watu wenye ulemavu kwa kuingiza matarajio na hali ya uhalisia wa watu wenye ulemavu katika mazingira yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sightsavers Bw.Godwin Kabalika ameeleza namna mradi huo wa uwezeshaji kiuchumi kwa watu wenye ulemavu ulivyotoa matokeo mazuri kwa nchi mbalimbali na ndio kwa mara ya kwanza mradi huo unaenda kutekeleza nchini Tanzania.
“Mradi huo umeshatekelezwa katika nchi ya Uganda,Kenya,Bangladesh ambapo mradi huo umezaa matunda ni matumaini yangu kupitia serikali itatuunga mkono kuhakikisha mradi huu unawafikia walengwa.
Hata hivyo Kabalika ameeleza sababu kubwa ya kuwepo mradi huo ni changamoto kubwa ya kupatikana kwa soko la ajira kwa watu wenye ulemavu na kupelekea jamii kuwaona watu hao ni “ombaomba “.
Aidha ameongeza kuwa mradi huo umeanzia mikoa ya Singida na Dar es salaam na una lengo la kuwafikia Mkoa wa Ruvuma,Lindi na Songwe .
Nae Mkurugenzi wa Shirika la Vijana wenye ulemavu (YOWDO) Rajabu Mpilipili ameongeza kuwa mradi huo utaenda kugusa Maeneo ya kilimo na kuongeza mnyororo wa thamani katika shughuli zao na kuwajengea uwezo wa kushiriki shughuli za kiuchumi.
” Tunatarajia kuwafikia walemavu 360 na kunufaika maeneo mbalimbali na kutekelezwa kwa majaribio kwa mikoa miwili singida na Dar es salaam ambapo tunategemea jamii itatupokea na kuwa mfano wa kuigwa kupitia mradi huo.
Pia ameeleza namna taasisi,vyama na Mashirika binafsi ya watu wenye ulemavu akilitaja (YOWDO,VODIWOTA DOLASED ) tayari yameonyesha dhamira ya dhati kuhakikisha mradi huo unafanikiwa na kuwafikia walengwa ifikapo 2025.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, akizungumza wakati akizundua Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi kwa Watu wenye Ulemavu unaotekelezwa na Taasisi ya Sightsavers kwa wanufaika 360 uliofanyika leo Mei 18,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sightsavers Bw. Godwin Kabalika akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi kwa Watu wenye Ulemavu unaotekelezwa na Shirika la Sightsavers kwa wanufaika 360 uliofanyika leo Mei 18,2023 Jijini Dar es Salaam.
Meneja Miradi wa Shirika la Sightsavers Bw.Edwin Maleko akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi kwa Watu wenye Ulemavu unaotekelezwa na Shirika la Sightsavers kwa wanufaika 360 uliofanyika leo Mei 18,2023 Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu Wenye Ulemavu, Oliver Njogopa akiungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi kwa Watu wenye Ulemavu unaotekelezwa na Shirika la Sightsavers kwa wanufaika 360 uliofanyika leo Mei 18,2023 Jijini Dar es Salaam
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida, Patrick Kasango akiungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi kwa Watu wenye Ulemavu unaotekelezwa na Shirika la Sightsavers kwa wanufaika 360 uliofanyika leo Mei 18,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Patrobas Katambi (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi kwa Watu wenye Ulemavu unaotekelezwa na Shirika la Sightsavers kwa wanufaika 360 uliofanyika leo Mei 18,2023 Jijini Dar es Salaam