Featured Kitaifa

WIZARA YA VIWANDA YAWAKUTANISHA MAOFISA BIASHARA MIKOA KUJADILI RASIMU YA MWONGOZO WA UFANYAJI BIASHAR NCHINI

Written by mzalendoeditor
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Conrad Milinga, akizungumza wakati akifungua warsha ya Makatibu Tawala Wasaidizi  sekta ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji ngazi za Mikoa kwa ajili kuipitia rasimu ya mwongozo wa kuboresha mazingira ya biashara nchini jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara ,wizara ya uwekezaji na Biashara Sempeho Manongi, akizungumza wakati wa warsha ya Makatibu Tawala Wasaidizi  sekta ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji ngazi za Mikoa kwa ajili kuipitia rasimu ya mwongozo wa kuboresha mazingira ya biashara nchini jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia nada mbalimbali wakati wa warsha ya Makatibu Tawala Wasaidizi  sekta ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji ngazi za Mikoa kwa ajili kuipitia rasimu ya mwongozo wa kuboresha mazingira ya biashara nchini jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Conrad Milinga, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua warsha ya Makatibu Tawala Wasaidizi  sekta ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji ngazi za Mikoa kwa ajili kuipitia rasimu ya mwongozo wa kuboresha mazingira ya biashara nchini jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imekutana na Makatibu Tawala wasaidizi sekta ya Viwanda,biashara na uwekezaji ngazi za Mikoa kwa ajili kuipitia rasimu ya mwongozo wa kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.
Akifungua warsha jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Conrad Milinga, amesema nia ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara kuanzia ngazi za chini.
“Tunataka mapato lazima tutengeneze watu ambao watatupa mapato suala la kuamka asubuhi unakwenda kufunga biashara ya mtu, tunataka tumjengee uwezo aone ana wajibu gani kwa serikali lisiwe suala la kusukumana, mtusaidie kutoa elimu ilia one Ofisa biashara ni msaada,”amesema.
Aidha, amesema wataalamu hao wataangalia mpango wa kuboresha mazingira ya biashara ikiwamo kuangalia ukuaji wa sekta binafsi.
“Uwekezaji unaofanyika huko kwenye ngazi za mikoa na halmashauri ufikie malengo yaliyowekwa, sisi kama serikali ina majukumu yake inawezekana bado tuna mawazo yale ya zamani tunapoiona sekta binafsi bado tunaitazama kwa mtazamo hasi,”amesema.
Amesema Maofisa hao ni wasimamizi kwenye Mikoa na Halmashauri kuhusu sheria, sera, kanuni na taratibu.
“Wawekezaji wanaokuja ambao wanaitwa na Rais Samia hawawekezi hewani wanawekeza kwenye mikoa na halmashauri, hivyo tusipofanya vizuri tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu,”amesema.
Awali,Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara ,wizara ya uwekezaji na Biashara Sempeho Manongi amesema kuwa lengo la kuwaita watendaji hao ni ili kuwaelewesha na kuhamasisha ujengaji wa mazingira wezeshi ya kibiashara uwekezaji na Viwanda.
”Kikao kitafanyika kwa siku mbili kinacholenga kuwapa uelewa wa majukumu yao, mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na kupitia mwongozo huo ili kuufanyia maboresho.”amesena Bw.Manongi
Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mororgoro Beatrice Charles ,amesema kuwa muongozo huo unaenda kuwafanya kazi kwa uweledi na kwamba wataenda kuondoa vikwazo eneo la uwekezaji,na ujenzi wa viwanda itakayosaidia kuongeza mapato.

About the author

mzalendoeditor