Featured Michezo

YANGA SC YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA NBC 2022/23

Written by mzalendoeditor

KLABU ya Yanga SC imeweka rekodi ikitwaa ubingwa wa 29 Ligi Kuu Tanzania bara  Msimu wa 2022/23 baada ya kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Dodoma jiji mchezo uliopigwa uwanja wa  Azam Complex  jijini la Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Kennedy Musonda dakika ya 39,Mudathir Yahya akifunga bao mawili dakika ya 70,90 na Farid Mussa dakika ya 88.

Mabao ya Dodoma jiji yamefungwa na Collins Opare dakika ya 59 na Seif Karihe dakika ya 67.

Ushindi huo unaifanya Yanga SC kutetea tena ubingwa wa Ligi Msimu huu ikiwa imefikisha Pointi 74 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote  huku ikiwa imebakiwa na michezo miwili dhidi  ya Mbeya City na Tanzania Prisons itachezwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

About the author

mzalendoeditor