Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA, Mhandisi Exaudi Fatael,akizungumza wakati akifungua mkutano wa madiwani wa jiji la Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya maji jijini hapa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) uliofanyika leo Mei 12,2023 jijini Dodoma.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mhe. Prof Davis Mwamfupe,akizungumza wakati wa mkutano wa madiwani wa jiji la Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya maji jijini hapa ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) uliofanyika leo Mei 12,2023 jijini Dodoma.
Meneja wa EWURA Kanda ya Kati Mhandisi Martin Maurus,aakitoa neno la utambulisho wakati wa mkutano wa madiwani wa jiji la Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya maji jijini hapa ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) uliofanyika leo Mei 12,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya Madiwani wakifatilia Mkutano wa madiwani wa jiji la Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya maji jijini hapa kilichoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo Mei 12,2023 jijini Dodoma.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo,akitoa mada kwa Madiwani wa jiji la Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya maji jijini hapa kilichofanyika leo Mei 12,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA, Mhandisi Exaudi Fatael,akiwa katika picha ya pamoja na madiwani mara baada ya kufungua mkutano wa madiwani wa jiji la Dodoma kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya maji jijini hapa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) uliofanyika leo Mei 12,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MKURUGENZI wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi Exaudi Fatael,amewataka Madiwani wa Jiji la Dodoma kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa uvunaji wa maji ya mvua kutokana na hali ya upatikanaji wa maji kwenye jiji hilo kutoridhisha.
Mhandisi Fatael ameyasema hayo leo Mei 12,2023 jijini Dodoma ,wakati akifungua mkutano wa madiwani hao kuhusu umuhimu wa matumizi ya vyanzo mbadala vya maji jijini hapa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Mhandisi Fatael amesema kuwa pamoja na hatua ambazo EWURA imeendelea kuchukua, hali ya upatikanaji wa maji jijini Dodoma, imekuwa si ya kuridhisha na kwamba Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa sasa ina vyanzo vya maji vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita miliomi 67.1 kwa siku wakati mahitaji ya maji kwa siku ni lita milioni 133.844.
“Hii inapelekea upungufu wa lita milioni 66.744 ya mahitaji ya maji kwa siku. Hata hivyo asilimia 28 ya maji yanayozalishwa hupotea. Kutokana na upungufu huo na maji yanayopotea, huduma ya maji inapatikana kwa wastani wa saa 10 tu kwa siku,”amesema Mhandisi Fatael
Aidha amesema kuwa vyanzo vya maji katika Jiji la Dodoma ni visima virefu ambavyo uzalishaji wake hautoshelezi mahitaji hivyo maji hutolewa kwa mgao kwa wastani wa saa 12 kwa siku.
Mhandisi Fatael,amesema kuwa utekelezaji wa suala hilo unahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali kama Mamlaka za Serikali za Mtaa katika kutafuta suluhu ya kuimarisha hali ya huduma ya maji.
“Madiwani wanayo nafasi ya kutunga sheria ndogo ndogo, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wake na kutoa elimu, inatoa rai kwenu, madiwani, kutoa hamasa kwa wananchi mnaowasimamia katika maeneo yenu, kuweka mikakati ya kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua, wakati hatua mbalimbali za kuimarisha huduma ya maji zikiendelea kuchukuliwa na DUWASA,”amesema
Awali Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mhe. Prof Davis Mwamfupe,amesema kuwa Jiji litahakikisha linatumia elimu hiyo ya EWURA ili wananchi kuona thamani ya kila tone la maji na kuyavuna.
”Sisi kama Madiwani wa jiji la Dodoma tunawapongeza EWURA kwa kutoa semina hiyo na tunawaahidi kuwa tutaenda kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuona thamani ya kila tone la maji na kuyavuna”amesema Prof.Mwamfupe