Featured Kitaifa

KIOTA KIPYA CHA KISASA KABISA ‘FK LODGE’ KIMEZINDULIWA MKOANI TABORA

Written by mzalendoeditor

 
Lodge
mpya ijulikanayo kama FK lodge imezinduliwa mkoani Tabora na Mwakilishi
wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo. Lodge
hiyo ya kisasa yenye vyumba 13 itaongeza upatikanaji wa malazi kwa
wageni wa ndani na nje ya nchi wanaotembelea Mkoani hapo kwa sababu
mbalimbali

Akiongea wakati wa Uzinduzi Mkurugenzi Mkuu wa FK
Lodge , Bwana Frederick Kanga amesema maono ya kuwekeza Tabora yameenda
sambamba na kukuwa kwa haraka kwa mkoa Tabora hususani kwenye miundo
mbinu ya Reli ya kisasa ambayo ikikamilika itaongeza mzunguko wa fedha
na shughuli mbalimbali za kiuchumi kipindi cha ujenzi na hata baada ya
reli kukamilika. 

 
Uwepo
wa barabara nzuri na za lami zinaziunganisha mikoa mingi ya jirani kama
shinyanga , Singida, Mbeya, Kigoma, Katavi na Sumbawanga pia kutafanya
Tabora kuwa kitovu cha biashara lakini pia kumekuwa na uhaba wa sehemu
za malazi zinazoshabihiana na kasi hii ya ukuaji na maendeleo na hivyo
tumeona ni vyema kuwekeza kwenye lodge ili kwenda sambamba na mahitaji
haya muhimu.
 
 Aidha
uwekezaji huu utawezesha kuwepo kwa ajira kwa wakazi wa Tabora na Mikoa
ya Jirani na hivyo kuchangia katika kukua kwa uchumi wa mkoa huu na
nchi kwa ujumla

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mwakilishi wa
Mstahiki Meya , Mh Molo Juma Molo Awapongeza sana wakurugenzi na
wamiliki wa FK Lodge kwa kuwekeza Tabora na kuahidi kutoa ushirikiano
katika kukuza na kuwepo kwa mazingira bora ya uendeshaji wa biashara na
kutoa wito kwa wadau wengine hususani wawekezaji wa ndani kuwekeza
katika Mkoa wa Tabora.

Akiongea huduma zinazopatikana Makamu
Mkurugenzi wa FK Lodge , Bi Jane Matinde Kanga amesema lodge hii ina
vyumba 13 vyenye huduma zote muhimu ikiwemo WiFi , lakini huduma za
vyakula na vinywaji pia vinapatika katika lodge hii. Aliongeza kwa
kusema”Tunajisikia fahari kuweza kutengeneza Ajira kwa vijana 9
zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi , kadhalika tumeingia mikataba
makapuni mbalimbali ya kutoa huduma kama za broadband, ulinzi, maji ,
umeme na hivyo kuchangia katika ungezeko la mapato yao na hivyo kukuza
uchumi na pato la taifa kupita kodi. Matumaini na maono yetu kuwa kuwepo
kwa lodge hii ni mwanzo wa nyingine nyingi katika maeneo mbalimbali
nchini”.

Kupata taarifa zaidi tembelea tovuti ya FK Lodge :

Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga akiongea wakati wa uzinduzi wa FK lodge iliyopo Ipuli Tabora

Mgeni
Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo
Juma Molo na Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga
wakikata keki wakati wa uzinduzi wa FK Lodge Tabora

Wafanyakazi
wa FK Lodge wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkurugenzi wa FK
Lodge , Bi Jane Matinde Kanga wakati wa Uzinduzi wa Lodge hiyo

Wamiliki wa FK Lodge Bwana na Bibi Frederick Kanga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa lodge mkoani Tabora

Mgeni
Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo
Juma Molo akiangalia muonekano wa lodge ndani wakati wa uzinduzi wa
lodge hiyo

Mgeni
Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo
Juma Molo akiangalia muonekano wa lodge ndani wakati wa uzinduzi wa
lodge hiyo

Wadau wa FK Lodge Joe na Mikidadi wakifungua champaign wakati wa uzinduzi


Wageni waalikwa wakipata chakula cha pamoja wakati wa uzinduzi

Baadhi ya wafanyakazi wa Exim walihudhuria uzinduzi wa FK Lodge mkoani Tabora

About the author

mzalendoeditor