Featured Kitaifa

MZUMBE KUZIDI KUENDELEZA BUNIFU ZAO NA KUZITAFUTIA MASOKO

Written by mzalendoeditor

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha,akizungumza na watumishi wa chuo hicho  katika banda la chuo hicho katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya  wiki ya ubunifu  2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha  wakati akizungumza na waandishi wa habari  katika banda la chuo hicho katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya  wiki ya ubunifu  2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa chuo hicho wakati wa  kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya  wiki ya ubunifu  2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

CHUO Kikuu cha Mzumbe kimesema kitaendelea kuibua,kuendeleza na kuzitafutia masoko bunifu mbalimbali zinazoibuliwa na wanafunzi wa chuo hicho huku kikidai   tayari ina  kitengo maalum kwa kusimamia bunifu hizo.

Hayo yameelezwa  na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha  wakati akizungumza katika banda la chuo hicho katika maonesho ya  wiki ya ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Prof Mwegoha amesema wanayafurahia maonesho hayo kwani yanahamasisha bunifu mbalimbali pamoja na masuala ya Sayansi na Teknolojia.

Amesema Mzumbe  wanachokifanya ni kuhakikisha wanapromoti bunifu mbalimbali za wanafunzi wao ambapo amedai kwa sasa wana Kitivo cha Sayansi na Teknolojia.

Amesema katika mambo wanayofanya katika kitivo hicho ni pamoja na wanafunzi kuja na bunifu mbalimbali ambazo zinaenda kutatua changamoto za wananchi.

Amesema bunifu ambazo wamekuja nazo ni  kwa ajili ya kupambana na changamoto za afya,mazingira,usafirishaji na uchukuzi.

“Sasa hivi tuna kitengo maalum kabisa kwa ajili ya kusimamia bunifu,baada ya hapa hawa vijana ili zile waweze kuzitangaza zifike mahali ambako  wataweza kutengeneza biashara ambazo zitawainua kiuchumi.

“Hii inaendana  na sera ya kitaifa ya kuhakikisha kwamba vijana wanajiajiri vijana wanaokuja hapa wanakuja na mawazo yao na tunawapa ushuri na baadae  kuzigeuza kuwa biashara ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wafanadhili ambao watazikuza,”amesema Prof Mwegoha

Amesema kupitia kituo hicho cha ubunifu wameanza  kwenye kituo atamizi ambacho kinawataalamu kwa ajili ya kukuza idea zao.

Amesema chuo kinakiwezesha  kitengo hicho  ili kuendeleza miradi na  waendelee kuwepo na kuwafikisha katika ndoto zao.

“Tutaendelea kuzisapoti mpaka pale ambapo wanaweza kuziendeleza na kuwa fursa.Hata wakiamua kwenda kufanya hizo kazi wana mahali pa kuanzia,”amesema Prof Mwegoha

Amesema katika bunifu walizokuja nazo ni pamoja na jiko ambalo linatumia mkaa wa  taka kwa ajili ya kulinda mazingira.

“Katika bunifu ambazo tumekuja nazo ni jiko ambalo linatumia mkaa wa taka kwa ajili ya nishati na  hii ni moja ya bunifu ambazo zipo nyingi ili serikali ikipiga marufuku mkaa tuweze kusapoti, majiko yanatumia taka lakini yanatoa nishati kubwa,”amesema Prof Mwegoha

About the author

mzalendoeditor