Featured Kitaifa

KATAMBI AWATAKA WATANZANIA KUJIUNGA NSSF.

Written by mzalendoeditor

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye  Ulemavu Patrobas Katambi akizungumza kwenye Banda la NSSF kwenye maonyesho ya maadhimisho ya siku ya kitaifa ya usalama mahala pa kazi yaliofanyika Mjini Morogoro.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye  Ulemavu Patrobas Katambiakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi WA NSSF.
NA FARIDA MANGUBE MOROGORO 
Naibu waziri, ofisi ya waziri mkuu – kazi, vijana, ajira na wenye enye ulemavu Patrobas Katambi amewataka Waajiliwa wa sekta binafsi na sekta isiyo Rasmi hasa wajasiriamali kujiunga na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) ili kujiwekea akiba Kupata fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoratibiwa na mfuko huo.
Naibu waziri Katambi ameyasema hayo kwenye maonyesho ya maadhimisho ya siku ya kitaifa ya usalama mahala pa kazi, Mjini Morogoro yalioratibiwa na Wakala wa usalama na afya mahala pa kazi (OSHA).
Akizungumza alipotembelea banda la mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii NSSF kujionea namna mfuko huo unavotekeleza majukumu yake ya usalama na afya mahala pa kazi amesema ni vyema watanzania Wote wenye sifa za kujiunga na mfuko huo wajiunge.
Aidha Naibu waziri Katambi amepongeza jitihada za NSSF kwa kuboresha huduma kwa Kutoa huduma kimtandao hali inayowalaishia wateja wake Kupata Taarifa wakati wowote.

About the author

mzalendoeditor