Featured Kitaifa

GGML YAIBUKA MUONYESHAJI BORA KATIKA MAONYESHO YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI 2023

Written by mzalendoeditor

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo Afisa Uhusiano wa GGML, Doreen Denis baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi ya kundi la muoneshaji bora katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea mkoani Morogoro.

Baadhi ya wafanyakazi wa GGML, wakiwa katika picha ya pamoja kufurahia ushindi wa muonesha bora na mbunifu bora katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayofanyika mkoani Morogoro.

Afisa Uhusiano wa GGML, Doreen Denis (kushoto) akimfafanulia jambo mwananchi aliyetembelea banda la maonesho la kampuni hiyo katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro. Wapili kushoto ni Afisa Mawasiliano Afisa Mawasiliano mwandamizi wa GGML, Laurian Theophil Pima.

Daktari wa Kituo cha Afya cha GGML kutoka Idara ya Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo ya GGML, Dk. Subira Joseph akitoa huduma za matibabu kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la huduma za afya la kampuni hiyo kwenye maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayofanyika mkoani Morogoro.

KATIKA maadhimisho ya siku ya afya na usalama mahali pa kazi  yanayoratibiwa na Wakala wa afya na usalama mahali pa kazi (OSHA), Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetangazwa muonyeshaji bora (Overall best exhibitor) miongoni mwa kampuni zote zilizoshiriki maonyesho hayo mjini Morogoro

Pia imetangazwa kuwa mbunifu bora wa maonesho hayo yaliyoanza Aprili 26 na kutarajiwa kuhitimishwa Aprili 30 mwaka huu katika viwanja vya Tumbaku mkoani humo.

Kilele cha maonesho hayo yenye kauli mbiu Mazingira Salama na Afya ni Kanuni na Haki ya Msingi Mahali pa Kazi.” kimefanyika jana mkoani humo.

About the author

mzalendoeditor