Featured Kitaifa

CPB YATANGAZA FURSA KWA WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA WA MAZAO

Written by mzalendoeditor

Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Salum Awadh akiongea na wadau (awapo pichani) katika kikao cha wadau wa Mazao kilichofanyika Jana katika Ukumbi wa Gentle Hill Iringa.

Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( CPB) Evans Mwanibingo akizungumza na wadau wa mazao ( hawako pichano), katikq kikao cha wadau hao kilichofanyika katika ukumbi wa Gentle Hill Iringa.

Kutoka Kushoto ni Meneja wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( CPB) Kanda ya Nyanda za juu Kusini Jasper Samwel,kaifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya CPB Salim Awadh wa mwisho ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Elia Luvanda wakifuatilia kikao cha wadau wa mazao kilichofanyika katika ukumbi wa Gentle Hill Iringa.

Wadau wa mazao wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha wadau kilichoandaliwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko

Na Mwandishi wetu.Iringa.
MWENYEKITI wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Salum Awadh ametangaza fursa mbalimbali zinazotolewa na CPB kwa wakulima na wafanyabiashara wa Mazao hapa nchini.

Aidha Awadh alitaja baadhi ya fursa zinazotolewa na CPB ni pamoja kilimo cha mkataba ambacho kitaanzia na hekali 1000 na kuendelea.

Akizungumza katika kikao cha wadau kilichofanyika leo Iringa Awadh alisema Kilimo cha mkataba CPB kitakuwa na uwezo mkubwa kutoa maelekezo na ufuatiliaji kwa urahisi.

” Kilimo cha mkataba kitasaidia kuwa na uhakika wa wakulima watakaotuletea mazao, yatakuwa katika ubora”‘ alisema Awadh.

Mwenyekiti huyo alisema fursa zingine ni pamoja na kuhitaji Mawakala ambao wataingia nao mkataba kwaajili ya uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa CPB na kununua mazao kutoka kwa wakulima na wafanyabishara.

Awadh alisema CPB ni Shirika la Kibiashara la Serikali hivyo linafanya biashara kwa lengo la kuinua Uchumi wa Nchi lakini na mtu mmoja mmoja.

“Biashara ambayo CPB inafanya hatuwezi kumlalia mkulima au mfanyabiashara wa mazao, Sisi lengo letu, Sisi tupate na nyie mpate,alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi.

Aidha Awadh alisema CPB ina maghala ambayo hutumia kuhifadhia mazao na bidhaa zao, hivyo wanafanya pia biashara ya kuhifadhi mazao katika maghala hayo ambayo yapo katika Mikoa mbalimbali.

vilevile Mwenyekiti huyo alisema kuwa CPB pia inatafuta masoko kwa Wakulima kama wanunuaji lakini kuwatafutia wakulima na wafanyabiashara kuwa inganisha na masoko ya nje.

Aidha Awadh alisema CPB inaongezea thamani mazao kwa kuchakata mazao kama Mpunga, Mahindi, Ngano, Alizeti na Siagi kupitia Viwanda vya CPB vilivyopo katika baadhi ya Mikoa ikiwemo Iringa.

Mwenyekiti huyo amewataka wafanyabiashara na wakulima wa mazao watumie fursa hiyo ili kuinua uchumi wao.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema katika kujiimarisha katika uchakataji wa mazao wanatarajia kujenga viwanda vingi zaidi katika Mikoa mbalimbali.

Awadh alitaja Mikoa ambayo tayari kuna viwanda vya kuchakata mazao kuwa ni , Dodoma ambapo kuna kiwanda cha kuchakata Mahindi na Alizeti.

Alitaja Mikoa mingine kuwa Arusha kuna kiwanda cha kuchakata Mahindi na Ngano, Iringa kiwanda cha kuchakata Mahindi, Mwanza kiwanda cha kuchakata Mpunga na Dar eslaam kuna Kiwanda cha kuchakata Siagi ya Korosho.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Elia Luvanda ambaye alifungua kikao hicho aliitaka CPB kuangalia uwezekano wa kujenga kiwanda cha unga wa lishe kwaajili ya wanafunzi mashuleni.

“Unajua ukanda huu wa Nyanda za juu kuna tatizo la watoto kukosa lishe,hivyo niwaombe CPB mbali na kufanya biashara ya mazao,wajenge kiwanda cha kutengeneza lishe ili watoto wetu waondokane na utapiamlo’, alisema Luvanda.

About the author

mzalendoeditor