Featured Magazeti

TAEC YASHIRIKI WIKI YA UBUNIFU 2023 JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Na .Alex Sonna-DODOMA

 

TUME ya nguvu za Atomiki nchini (TAEC) ,imetakiwa kuwekeza zaidi katika utafiti ili kupata bunifu nyingi hasa kwenye eneo la Sayansi ya Nyuklia kwani ni muhimu sana katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

 
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ,teknolojia na Ubunifu Prof Maulilio Kipanyula , leo Jijini Dodoma kwaniaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu wakati wa Siku ya Atomiki kwenye maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 iliyoambatana na maandamano yaliyofanyika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

 

 

 
“TAEC mna kazi kubwa sana ya kuhakikisha mnafanya tafiti zaidi kwenye eneo la sayansi ya Nyuklia kwani karibia ulimwengu wote sasa umegekia huko na lengo ni kukuza uchumi wa nchi na naamini kupitia maonesho haya wananchi watapata nafasi ya kuijua zaidi tume hii,”
 
 
Na kuongeza kuwa “Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni moja ya taasisi muhimu sana katika taifa letu kwa sababu inagusa sekta nyingi sana ukianzia kwenye sekta Afya mionzi inatumika ,kwenye chakula,mbegu na maeneo mengine mengi hivyo ni muhimu sana kuongeza tafiti na wanachi waelimishwe zaidi kuhusu majukumu ya taasisi hii,”amesema Prof.Kipanyula
  

 

 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Tume hiyo,Prof Joseph Msambichaka ameitaka tume ya Atomiki kufanya bunifu nyingi zinazotokana na nyuklia kwani Tume hiyo ina uhitaji wa vifaa vingi vyakutosha.
 
 
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Prof Lazaro Busagala amesema kuwa hapo baadae wanatarajia kuwa na uwakilishi mkubwa wa wanawake katika sayansi na teknolojia hasa ya Nyuklia ambapo hivi sasa wametenga jumla ya Shilingi bilioni 2.6 kwaajili ya kuwasomesha wanafunzi ambao wamefanya vizuri katika shahada zao kupitia mpango mkakati wa Dkt. Samia scholarship ili kupata wabunifu zaidi.

 

 “Tuna mpango wa kuwapeleka wanafunzi watano katika vyuo mbalimbali Duniani kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusu matumizi ya Nguvu za Atomiki katika nyanja mbalimbali.

 
 
Maonesho hayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kushirikisha ni Taasisi za Elimu ya Juu, Taasisi za Utafiti na Maendeleo, Vyuo vya Ufundi, Mashirika na Taasisi za Umma, Mashirika na Taasisi binafsi za teknolojia, Wizara mbalimbali na Wabunifu walioendeleza katika programu ya MAKISATU na kufikia hatua ya ubiasharishaji.

 

 

 
Lengo likiwa ni kuwakutanisha wabunifu mbalimbali ambapo wanatumia maonesho hayo kama jukwaa la kuonesha bidhaa zao mpya ambazo wamezibuni kupitia Taasisi zao ili jamii ione na kuvichukuwa kwa ajili ya kwenda kuvitumia kwa kutatua changamoto zao na kurahisisha utendaji katika shughuli za kila siku.

About the author

mzalendoeditor