Spika wa Bunge la Tanzania atembelewa na wageni wabunge kutoka Uganda (baadhi) leo tarehe 24 Aprili 2023 katika ukumbi wa Spika jijini Dodoma
Aidha, Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) alipokea maswali na kuwajibu kuhusu uendeshaji wa shughuli za Bunge, kazi za Spika na taratibu za Mikutano ya Bunge kwa ujumla
Kabla ya kukutana na Spika, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ndg.Daniel Eliufoo aliwapa historia ya Bunge la Tanzania, Muundo wa Bunge na kuwaelezea kazi za Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Bungeni.
Baada ya ziara hii kwa leo walimshukuru Mheshimiwa Spika kwa ukaribisho mzuri na kumtaarifu kuwa Uganda wanampenda sana na wanamtumia salamu nyingi.
Wageni hawa wapo kwenye ziara kuanzia tarehe 23 hadi 28 Aprili 2023