Featured Michezo

YANGA SC YATANGULIZA MGUU NUSU FAINALI,MAYELE APIGA MBILI

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna

WAWAKILISHI Pekee ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Timu ya Yanga SC wamelipa kisasi baada ya kuwachapa mabao 2-0 wenyeji Rivers United mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua Robo ya Fainali mchezo huo umepigwa katika uwanja wa  Godswill Akpabio nchini Nigeria.

Kipindi cha kwanza timu zote zilienda mapumziko zikiwa hazijafungana huku wenyeji wakimiliki mpira kutokana na Yanga SC kuanza na viungo wengi na mabeki.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko  yaliyoweza kuipa Yanga ushindi huo mnamo dakika ya 74 Mshambuliaji hatari kwa sasa ndani na nje ya nchi Fiston Mayele alifunga bao la kwanza akimalizia pasi ya Nahodha wake Bakari Mwamnyeto.

Rivers wakiwa wanawaza kusawazisha bao Yanga SC walipiga counter yule yule mtoa pasi Bakari Mwamnyeto alimpa tena Fiston Mayele dakika ya 81 na kufunga bao la pili likiwa bao lake la tano na kuwa kinara katika kufumania nyavu katika  Michuano hiyo

Kwa matokeo hayo Yanga SC imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga Nusu Fainali kwani inahitaji kulinda tu ushindi wake hata wakifungwa bao moja watafuzu hatua hiyo timu hizo zinatarajia kurudiana kati ya Aprili 29 au 30,mwaka huu.

Yanga watachukua sh.milioni 10 za Rais Samia Suluhu Hassan baada ya ushindi huo ambazo amekuwa akitoa kama motisha kwa kununua kila bao sh.milioni 5 katika hatua hiyo ya CAF.

About the author

mzalendoeditor