Featured Kitaifa

MSIGWA:RIPOTI YA CAG HAIZUI MIRADI YA KIMKAKATI KUENDELEA

Written by mzalendoeditor
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma hafla iliyoambatana na Iftar ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
SEHEMU ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Gerson Msigwa  (hayupo pichani) jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye hafla iliyoambatana na Iftar ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imesema kuwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inatumika kama Nyenzo kwa serikali ili kuhakikisha yale mapungufu yote yaliyobainika yanafanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari iliyoambatana na Iftar ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Msigwa amesema kuwa Serikali ipo kazini na hakuna mradi wowote uliosimama au utakaosimama kwa sababu yeyote ile hivyo miradi ya maendelei inazidi kuchanja mbuga.

“Niwatoe hofu wananchi, ripoti ya CAG ni nyenzo inayotumiwa na Serikali kusimamia rasilimali za watanzania,hivyo niwahakikishie kupitia ripoti hiyo Serikali ipo macho kulinda na kutetea rasilimali,achaneni na taarifa za mitandaoni zinazokatisha tamaa,”amesema.Bw Msigwa
Hata hivyo Msigwa amewata wananchi kuachana na mijadala ya ripoti hiyo ambayo imejaa  upotoshaji na isiyojenga yenye lengo la kuharibu taswira ya nchi na badala yake wajikite kwenye ujenzi wa Taifa .
Kuhusu miradi ya kimkakati Msigwa amesema mwendo ni uleule hakuna kilichobadilika wala kusimama na kutolea mfano mradi wa reli Morogoro -Makutopora kuwa unaendelea kutekelezwa ukiwa umefikia asilimia 93.3.
“Miradi yote ya kimkakati inaendelea kutekelezwa, Serikali ya Rais Samia Ina nia ya dhati na itahakikisha mipango yote inatekelezwa ikiwemo mabehewa ya ghorofa,mradi wa uzio wa Tembo ambao umeanza Kwa mara ya kwanza nchini na barabara ya mzungu ya Dodoma ambayo imefikia asilimia 18.

Aidha Msigwa amewataka waandishi wa habari kuendelea na kazi zao bila wasiwasi kwani serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan inatambua, inadhamini na itaendelea kusimamia uhuru wa vyombo vya habari.

“Chapeni kazi kwa kuzingatia sheria penye changamoto tushirikishane ili tuweze kuzitatua na jueni tu serikali inatambua sana kazi zenu,”amesema Msigwa

About the author

mzalendoeditor