Featured Kitaifa

MGANGA MKUU WA SERIKALI ATETA NA MWAKILISHI WA UBALOZI WA IRELAND NCHINI

Written by mzalendoeditor

 

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu leo Tarehe 19/4/20223 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania Dkt. Peter Nyella.

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano katika kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini hususan katika maeneo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika fani za ubingwa na ubingwa ubobezi na Ubora wa huduma

Aidha mwakilishi huyo ameambatana Prof. David Weakliam na ujumbe wa wawakilishi wa Wizara ya afya nchini Ireland.

About the author

mzalendoeditor