WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye,akishuhudia utiaji saini kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mhandisi Peter Ulanga,(Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji HUAWEI ,Bw.Demong Zhang,wakisaini Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati TTCL na HUAWEI hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mhandisi Peter Ulanga,wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye,akiuliza Swali mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mhandisi Peter Ulanga,wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
KAIMU Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bi.Salome Kessy,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bi.Zuhura Sinare Muro,akielezea mikakati yao katika kuimarisha miradi ya Mkongo wa Taifa wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mhandisi Peter Ulanga,akitoa maelezo wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji HUAWEI ,Bw.Demong Zhang,akielezea watakavyofanya kazi kwa haraka ili wananchi waweze kupata huduma bora wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) ,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye,akishuhudia utiaji saini kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mhandisi Peter Ulanga,(Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji HUAWEI ,Bw.Demong Zhang,wakisaini Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati TTCL na HUAWEI hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mhandisi Peter Ulanga,(Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji HUAWEI ,Bw.Demong Zhang,wakionyesha Mkataba mara baada ya kusaini Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati TTCL na HUAWEI hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushuhudia utiaji Saini wa Mkataba wa Upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Wilaya 23 uliosainiwa kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na HUAWEI International Co. Limited hafla iliyofanyika leo Aprili 17,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imesaini mkataba wa upanuzi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika wilaya 23 nchini, wenye urefu wa kilomita 1,520 utakao gharimu zaidi ya Sh. bilioni 37 na utatekelezwa kwa muda wa miezi sita.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utilianaji saini kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania na Kampuni ya HUAWEI Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe Nape Nnauye,amesema kukamilika kwa mradi huo kutaleta mageuzi makubwa katika ukuaji wa maendeleo ya Taifa.
Amesema Kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa kwa wananchi za kiuchumi, kwani Kasi ya upatikanaji wa mawasiliano yatachochea maendeleo Katika Wilaya hizo na Taifa kwa ujumla.’
“Mradi huu wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano utasaidia kukuza matumizi ya TEHAMA na kuongeza kasi upatikanaji wa Intaneti yenye kasi, mawasailiano yatasaidia wilaya kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa kutumia mifumo ya kidijitali”amesema Nape
Aidha amesema Serikali kwa kutambua changamoto za wilaya zetu za kukosa mawasiliano ya uhakika ambayo yamesababisha wananchi katika wilaya hizo kukosa fursa mbalimbali za kijamii na kibiashara.
“Serikali imepanga kutekeleza mradi wa kuimarisha mawasiliano katika ngazi ya wilaya kwa kuunganisha wilaya zote kwenye mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa mawasiliano ambayo yatachochea maendeleo katika wilaya hizo na Taifa kwa ujumla”amesisitza Nape
Ameongeza kuwa “Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na miundombinu bora ya mawasiliano yenye kutumia teknolojia ya kisasa ambayo italeta tija na ufanisi katika kuongeza uzalishaji na ujenzi wa uchumi wetu na kuimarisha usalama na ulinzi wa Taifa letu”
Vilevile, amesema mawasiliano hayo yatasaidia serikali kufikisha utekelezaji wa Tanzania ya kidijitali hadi ngazi ya wilaya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bi.Zuhura Sinare Muro, ameishukuru Serikali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuwezesha utekelezaji wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenda kwenye ngazi ya Wilaya.
”Leo ni siku muhimu kwa Shirika letu na Taifa kwa ujumla kwa uwekezaji huu ambao unaenda kuimarisha sekta ya mawasiliano Nchini na kuchangia katika kukua kwa sekta nyingine za maendeleo”amesema Bi.Muro
Aidha amesema kuwa Upanuzi huu wa Mkongo wa Taifa unakwenda sambamba na Dira na Malengo ya Shirika katika kuhakikisha inakuwa mtoa huduma bora wa miundombinu ya mawasiliano data na simu Kitaifa na Kimataifa.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),Mhandisi Peter Ulanga, amesema kuwa mkataba huo uliosainiwa unatakiwa kukamilika ndani ya miezi sita tangu kusainiwa kwake.
“Kukamilika kwa mradi huo kutaondoa tatizo lililokuwepo awali la ukosefu wa mawasiliano katika wilaya hizo.”amesema Mhandisi Ulanga