Featured Kitaifa

RC SENYAMULE AFUTURISHA UZUNGUNI DODOMA

Written by mzalendoeditor

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na viongozi na makundi mbalimbali ya watu walioshiriki katika hafla ya Iftar ya pamoja iliyoandaliwa na Ofisi yake nyumbani kwake Uzunguni Jijini Dodoma tarehe 16/04/2023.

Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Mhe.John Mongella (Mgeni Maalumu) akizungumza na viongozi na makundi mbalimbali ya watu walioshiriki katika iftar ya pamoja iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Dodoma

Mhe. Rosemary Senyamule katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu baada ya Iftar ya pamoja iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkoa

Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika Iftar ya pamoja iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Dodoma nyumbani kwake Uzunguni Jijini Dodoma

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Shabaan akitoa neno kwa washiriki wa Iftar iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Uzunguni Jijini Dodoma

Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameungana na Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa taasisi za Umma, Viongozi wa Serikali, Wabunge, Madiwani, Baraza la wazee , wafanyabiashara ,sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa vyuo, Machifu, wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Makundi mbalimbali  na kupata iftari ya pamoja aliyoiandaa nyumbani kwake Uzunguni.

Katika iftari hiyo iliyoongozwa na Mgeni Maalimu Mkuu wa Mkoa Arusha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mkoa Mhe. John Mongela pia ilihudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Sheikh Mustapha Shabaan, pamoja na kulenga  kutoa sadaka na kukuza mahusiano mema baina ya wananchi na viongozi  katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan pia ili lenga kumuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Senyamule ametoa salamu za shukurani kwa viongozi mbalimbali wa dini, serikali na wananchi waliofika  kwenye  iftari hiyo kwa kufanikiwa kujumuika pamoja katika tukio lilalojenga umoja, amani na mshikamano miongoni mwajamii. 

“Tuliona kama Mkoa ni nafasi nzuri ya kukaa na nyie pamoja na kula chakula hiki  lakini kuwapongeza kwa kazi ambayo mmekuwa mkifanya katika kipindi hichi cha mfungo, najua ukiwauliza watu kwenye mfungo unafanya nini wanasema tunafanya toba kwa Mwenyezi Mungu atupe rehema kwa mambo tuliyo mkosea, maombi maalum kwa ajili ya mambo ambayo tuna yahitaji kama familia, Viongozi na Taifa “Amesema Senyamule 

Hafla hiyo ya iftari imehudhuriwa na Naibu Waziri na Mbunge wa Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde, Wabunge wa Viti maalumu, Wakuu wa Wilaya,Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma.

About the author

mzalendoeditor