Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa viungo bandia, iliyoratibiwa wa Taasisi ya Narayan Seva Santhan ya India na Cello Industries (T) LTD, ambapo Watu wenye Ulemavu 178 wamepatiwa viungo bandia.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo ya ugawaji wa viungo bandia iliyoratibiwa wa Taasisi ya Narayan Seva Santhan ya India na Cello Industries (T) LTD, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiangalia Mguu wa Bandia wakati wa hafla hiyo iliyoratibiwa wa Taasisi ya Narayan Seva Santhan ya India na Cello Industries (T) LTD, ambapo Wenye Ulemavu 178 wamepatiwa viungo bandia.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akikabidi mguu wa bandi wakati wa hafla hiyo iliyoratibiwa wa Taasisi ya Narayan Seva Santhan ya India na Cello Industries (T) LTD, ambapo Wenye Ulemavu 178 wamepatiwa viungo bandia, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa kwenye picha ya pamoja na Watu wenye Ulemavu akati wa hafla hiyo iliyoratibiwa wa Taasisi ya Narayan Seva Santhan ya India na Cello Industries (T) LTD, ambapo Wenye Ulemavu 178 wamepatiwa viungo bandia, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametoa rai kwa wadau kuwa na utaratibu wa kutoa viungo bandia na vifaa saidizi kwa ajili ya ustawi wa Watu wenye Ulemavu.
Profesa Ndalichako amebainisha hayo Aprili 15, 2023 jijini Dar es salaam, wakati wa hafla ya ugawaji wa viungo bandia, chini ya uratibu wa Taasisi ya Narayan Seva Santhan ya India na Cello Industries (T) LTD, ambapo Watu wenye Ulemavu wapatoa 178 wamepatiwa viungo bandia.
“Hatua hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mnaguswa na kundi hili na mnamuunga mkono Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae amekuwa kinara na mwenye dhamira ya kweli na maono makubwa katika kuleta ustawi kwa Watu wenye Ulemavu nchini”
Amesisitiza kuwa serikali tayari imetoa Tshs. 1,023,500,000 ili kuwajengea mabweni 8 katika Shule za Msingi nchini, Mwongozo wa Taifa wa Utambuzi wa Mapema na Afua Stahiki kwa Watoto wenye Ulemavu pamoja na Mwongozo wa Utekelezaji, Ujumuishwaji na Uimarishaji wa huduma kwa Watu Wenye ulemavu umeandaliwa.
“Niendelee kutoa wito kwa Watanzania wote kuacha mila potofu za kuwaficha Watoto wenye Ulemavu. Ni muhimu tuwaibue kupitia ngazi zote za Kijiji, Kata, Wilaya, Mikoa na Taifa na kuwaunganisha mapema na huduma za Marekebisho na Utengamao”
Kwa upande wa waratibu wa hafla hiyo Narayan Seva Santhan ya India na Cello Industries (T) LTD, wameishukuru serikali kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wenye ulemavu ambapo wameahidi kuendelea kuunga jitihada za serikali
Aidha, wamebainisha kuwa zoezi hilo limegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 38,100 kwa watu 178 kupatiwa viungo bandia. Vilevile watu wenye ulemavu 100 wamepatiwa Callipers kwa ajili ya viungo vilivyopinda.