Featured Michezo

AZIZ KI AITUMIA SALAMU SIMBA SC,APIGA HAT-TRICK

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna

MABINGWA Watetezi Yanga SC wameendelea kuukaribia Ubingwa wa 29 mara baada ya kuizamisha mabao 5-0 Kagera Sugar Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Chamazi Complex Azam nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Yanga walienda mapumziko wakiwa mbele ya mabao mawili yaliyofungwa na Kiungo Mshambuliaji Stephane Aziz Ki dakika ya 43 kwa Mkwaju wa Penalti na dakika 45 +1 akifunga kwa shuti kali nje ya 18 ambalo limemshinda kipa Said Kipao wa Kagera Sugar.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuendelea kulishambulia lango la Kagera Sugar na mnamo dakika 47 Fiston Mayele aliwanyanyua mashabiki wake baada ya kufunga bao safi likiwa la 16 Msimu huu na kuendelea kukaribia kuchukua kiatu cha mfungaji bora.

Akitokea benchi Kiungo Mtukutu Benard Morrison alipingilia msumari wa nne dakika ya 84 akifunga kwa shuti kali nje ya 18 ambalo limemshinda kipa Said Kipao wa Kagera Sugar,dakika ya 90 Stephane Aziz Ki akafunga bao la tano kwa Mkwaju wa Penalti na kuhitimisha Hat-Trick yake ya kwanza tangu ajiunge na Yanga

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 68 wakiwaacha watani zao Simba SC wenye pointi 60 na kuachwa kwa tofauti ya Pointi 8 ,Sasa watakutana siku ya Jumapili Aprili 16,2023 mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo mwingine umepigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wenyeji KMC jahazi limezidi kuzama baada ya kufungwa mabao 2-0 na Geita Gold FC

About the author

mzalendoeditor