Featured Michezo

YANGA SC YAIFUATA SIGINDA BIG STARS NUSU FAINALI YA ASFC

Written by mzalendoeditor

MABINGWA Watetezi Yanga  SC  wameifuata Timu ya Siginda Big Stars   Hatua ya Nusu Fainali Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold FC kutoka Mkoani Geita mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jijini Dar es Salaam.

Yanga SC walipata bao dakika ya 57 likifungwa na Mshambuliaji hatari kwa sasa nchini Fiston Mayele akimalizia pasi ya winga Tuisila Kisinda.

Sasa Yanga SCwatakutana na Singinda Big Stars ambayo iliichapa mabao 4-1 Mbeya City huku Simba SC itakutana na Azam FC katika mchezo wa Nusu wa Fainali.

Nusu Fainali hizo zitachezwa katika Mikoa ya Mtwara na Siginda na Fainali itachezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga jijini Tanga.

About the author

mzalendoeditor