TIMU ya Wasichana ya Shule ya Sekondari ya Fountain Gate ya Dodoma wameibuka mabingwa wa mshindano ya soka kwa shule za Afrika ya CAF,kufuatia ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa fainali dhidi ya Ecole Omar IBN Khatab ya Morocco leo Uwanja wa King Zwelithini Jijini Durban, Afrika Kusini.
Katika michuano hiyo iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Winfrida Hubert mawili na Irene Chitanda moja na huo ulikuwa mchezo wa pili leo baada awali kuitandika SCG De Mfilou ya Kongo mabao 4-0 katika Nusu Fainali.
Kwa kutwaa ubingwa huo, Fountain Fate imezawadiwa dola za Kimarekani 300,000, kiasi ambacho pia amepewa bingwa wa upande wa wavulana, huku washindi wa pili wakiondoka na dola 200,000 na wa tatu dola 150,000.