Featured Kitaifa

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA BODI, MENEJIMENTI YA REA KUJADILI UTENDAJI KAZI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nishati, January Makamba (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kujadili utendaji kazi wenye mlengo wa kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini. Kikao hicho kilifanyika Machi 29, 2023 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara, Mhandisi Felchesmi Mramba na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Janet Mbene.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Janet Mbene (aliyesimama), akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Nishati, January Makamba na Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Machi 29, 2023 jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilijadili utendaji kazi wenye mlengo wa kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Nishati, January Makamba na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti ya REA, Machi 29, 2023 jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilijadili utendaji kazi wenye mlengo wa kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) wakifurahia jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nishati, January Makamba na Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya REA, Machi 29, 2023 jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilijadili utendaji kazi wenye mlengo wa kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakifuatilia kikao cha Waziri wa Nishati, January Makamba na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti hiyo, Machi 29, 2023 jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilijadili utendaji kazi wenye mlengo wa kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati, Jacqueline Materu (kushoto) na Msafiri Baraza wakifuatilia kikao cha Waziri wa Nishati, January Makamba na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Machi 29, 2023 jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilijadili utendaji kazi wenye mlengo wa kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Na.Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

Waziri wa Nishati, January Makamba amefanya kikao na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kujadili utendaji kazi wenye mlengo wa kuboresha zaidi utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Katika kikao hicho kilichofanyika Machi 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam, Waziri alisema REA imekuwa ikifanya kazi nzuri lakini akaitaka kuongeza mbinu zitakazowezesha kuhakikisha miradi ya nishati vijijini inatekelezwa kwa ubora zaidi, kwa wakati na viwango.

Aidha, alisema kuwa miradi inayotekelezwa na REA inagusa maisha ya wananchi moja kwa moja hivyo inabidi itekelezwe kwa kuzingatia kupoza kiu yao na kuwapatia huduma iliyoahidiwa na Serikali kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi, Janet Mbene alimhakikishia Waziri kuwa Bodi itasimamia utekelezaji wa maagizo yote aliyoyatoa.

About the author

mzalendoeditor