Burudani Featured

BINGWA WA DUNIA WA BAISKELI ATAKA KUINGIA REKODI YA GUINESS KUPITIA MLIMA KILIMANJARO

Written by mzalendoeditor

 

 
 
Bingwa wa Kuendesha Baiskeli Duniani mara 5 mfululizo kutoka Poland Mike “Leszek” Mikulski @mikelmikulski ambaye yuko katika maandalizi kabambe ya kuweka rekodi ya Dunia ya Guiness kwa kupanda Mlima Kilimanjaro kwa baiskeli akitumia saa chache zaidi kuliko mwanadamu yeyote, leo amekutana na viongozi wa Wizara ya Utalii nchini katika kuona namna tukio hilo linavyoweza kuileta dunia hapa Tanzania.
Inakadiriwa zaidi ya watu 200, wakiwemo wanahabari wa kimataifa na majaji kutoka Kamati ya Dunia ya Guiness, watafuatana naye kuja nchini kushuhudia na kuithibitisha rekodi hiyo.
 

About the author

mzalendoeditor