Featured Michezo

MICHEZO YA MEI MOSI KUTIMUA VUMBI MOROGORO

Written by mzalendoeditor

Michezo Inayo wakutanisha wafanyakazi kutoka katika mashirikisho ya Micghezo ya Wafanyakazi wa Wizara, Mikoa, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali SHIMIWI), Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma na Makampuni Binafisi (SHIMMUTA), Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) na Wafanyakazi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (BAMMATA) maarufu MEI MOSI mwaka huu itafanyika Mjini Morogoro kuanzia tarehe 16 hadi 30 Aprili, 2023 ambako pia kilele cha Sherehe za wafanyakazi KiTaifa zitakakofanyika.

Michezo itakayoshindaniwa ni Mpira wa Miguu, Netiboli, Riadha, Kuvutana kwa Kamba, Karata, Bao, “Draft”, Baiskeli na Mpira wa Wavu (Volleyball), katika Viwanja vya Jamhuri, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Mazimbu, Shule ya Sekondari Morogoro, Kiwanda cha Tumbaku, Magadu na Chuo cha Ujenzi.
 
Hadi sasa Timu zilizo onyesha nia ambazo zipo katika maandalizi ya kushiriki ni ofisi ya Rais Ikulu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wizara ya Mambo ya nje, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Ulinzi na JKT, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wizara ya Maliasili na Benki ya CRDB. 
 
Tunaziomba timu zinazojiandaa kushiriki zithibitishe kwa maandishi kwa kutaja aina ya Michezo watakayoshiriki ili kamati iweze kupanga ratiba na kufanya maandalizi muhimu kama Viwanja na waamuzi kulingana na idadi ya timu.
 
 Aidha, tunasisitiza timu zote kufika katika kituo cha mashindano (Morogoro) ifikapo tarehe 14 Aprili, 2023. Timu itakayopangwa katika ratiba endapo itachelewa kufika na kukuta Mchezo/Michezo yake imepita itahesabika kuwa amepoteza Mchezo/Michezo  hiyo kwa mujibu wa kanuni za mashindano.
 
Tunawatakia maandalizi mema pia tunawakaribisha Mjini Morogoro.
“Mshikamano Daima”

About the author

mzalendoeditor