Featured Kitaifa

DKT.JINGU AIPONGEZA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII  KUANZA MCHAKATO WA MAPITIO YA MITAALA KWA WAKATI

Written by mzalendoeditor

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu,akizungumza wakati  akifungua Warsha ya Mapitio ya Mitaala ya programu ya uhandisi ujenzi na Maendeleo ya Jamii iliyofanyika leo Machi 27,2023 jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe na Washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu, wakati  akifungua Warsha ya Mapitio ya Mitaala ya programu ya uhandisi ujenzi na Maendeleo ya Jamii iliyofanyika leo Machi 27,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi Neema Mwakilembe,akitoa taarifa  wakati wa Warsha ya Mapitio ya mitaala ya uhandisi ujenzi na Maendeleo ya Jamii  iliyofanyika leo Machi 27,2023 jijini Dodoma.

Afisa Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Happy Hiza,akielezea umuhimu wa semina baada ya kumaliza  Warsha ya Mapitio ya mitaala ya uhandisi ujenzi na Maendeleo ya Jamii  iliyofanyika leo Machi 27,2023 jijini Dodoma.

Mkufunzi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Bw.Boniphace Daniel,akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza Warsha ya Mapitio ya mitaala ya uhandisi ujenzi na Maendeleo ya Jamii  iliyofanyika leo Machi 27,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

IDARA  ya Maendeleo ya Jamii imepongezwa kwa kuanza mchakato wa mapitio ya mitaala ya programu za Maendeleo ya Jamii na Uhandisi Ujenzi na Maendeleo ya Jamii kwa wakati.

Pongezi hizo zimetolewa leo Machi 27,2023 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu,wakati akifungua Warsha ya Mapitio ya mitaala ya uhandisi ujenzi na Maendeleo ya Jamii.

Dkt.Jingu amesema kuwa hatua hii itasaidia vijana wananojiunga na Vyuo vyetu pamoja na vyuo vyote vitakavyotumia mitaala hii wapate mafunzo yanayoendana na mazingira ya sasa.

” Niwashukuru NACTVET kwa jinsi ambavyo mmekuwa mstari wa mbele katika kutoa miongozo mbalimbali ya kuoboresha mafunzo. Vilevile ninawashukuru washiriki wote mliofika hapa kwa ajili ya kutoa maoni kwenye mitaala hii.”amesema Dkt.Jingu

Aidha Dkt.Jingu amewataka kuhakikisha mitaala watakayotumia kutoa mafunzo inaakisi hali halisi ya mazingira ya jamii yetu, na mahitaji ya nchi na Dunia kiujumla

”Mitaala ni lazima izingatie jamii imebadilika kiasi gani kufuatia mabadiliko ya kiteknolojia, kisiasa na kiuchumi yanatokea Duniania na hata nchini kwetu”amesema Dkt Jingu

 Dkt amesema kada ya Maendeleo ya Jamii inatazamiwa kuwa itachangia katika kuisukuma jamii mbele iwapo itazingatia uhalisia

“Kama jamii tunataka maendelea na maendeleo maana yake ni kwenda mbele kwahiyo mitaala hii itakua ni nyenzo muhimu kutufikisha huko niwaaombe tutekeleze vizuri tujidhatiti tuweke nguvu zetu, Akili zetu zote, Maarifa yetu yote ili likitoea hili na uhakika miaka mitano ijayo jinsi kada ya Maendeleo ya Jamii itakavyokua inasukuma Maendeleo Mbele” amesema Dkt. Jingu

Hata hivyo amewaagiza kuwa na mahusiano ya karibu baina ya wadau wa mitaala na vyuo hasa katika maeneo yao ili kuwezesha Taasisi hizo kuvuna wanafunzi ambao wana picha ya hali halisi ilivyo katika jamii.

“Nyie mkienda kule mnawasaidia kuwapa picha ya hali halisi ilivyo inawezekana mkiachia walimu waliopo pale wanawapa kwa nadharia ili baada ya hapo tutoke na mtu aliekamilia anauzoefu kupitia maarifa ambayo tunawagaia lakini vilevile ana nadharia ambazo zinahitajika,” amesema Dkt Jingu

Awali Mkurugenzi Msaidizi wa sehemu ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bi Neema Ndoboka amesema  jumla ya  washiriki 80 wameshiriki warsha hiyo.

”Mitaala ambayo inapitiwa ni Maendeleo ya jamii na Ufundi kwa ngazi ya cheti mpaka diploma ambayo iliandaliwa tangu mwaka 2018”amesema Bi.Neema

Naye mmoja wa washiriki Afisa Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Happy Hiza,amesema kuwa ni wakati sasa Mitaala kujumuisha Taaluma za kuwashawishi wananchi kushiriki katika utekelezaji wa Miradi ya serikali.

About the author

mzalendoeditor