Featured Kitaifa

WAKUU WA WILAYA MNADHAMANA KUBWA KULINDA KIZAZI CHA KITANZANIA- WAZIRI  GWAJIMA.

Written by mzalendoeditor

Na WMJJWM, DODOMA

Rai Imetolewa kwa Wakuu wa Wilaya nchini kuwa mstari wa mbele kubaini na kuibua mienendo isiyofaa ndani ya jamii ikiwemo vitendo vya ukatili na ukiukwaji wa Mila na Desturi zilizo nje na Utamaduni wa Mtanzania.

Akitoa mada kwa Wakuu wa Wilaya Machi 17, 2023 jijini Dodoma, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Viongozi hao ni nguzo muhimu katika Mapambano dhidi ya maovu ndani ya Jamii

Amewahimiza kuwatumia Maafisa Maendeleo na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanapata taarifa sahihi kwani watumishi wa Kada hiyo wapo karibu zaidi na jamii

“Utekelezaji wa Wizara hii una mchango mkubwa katika kutengeneza watu na Taifa hili kuanzia utoto wao hivyo mkiielewa Wizara hii na malengo yake na kuelezea vizuri kwa Jamii mtaongoza vizuri” amesema Dkt. Gwajima.

Mhe. Dkt. Gwajima amewasisitiza pia kuhakikisha NGOs zinazofanya kazi kwenye maeneo yao zinafuata mikataba, kanuni na sheria ikiwemo misingi ya maadili.

About the author

mzalendoeditor