Featured Michezo

SIMBA SC YASHTUA AFRIKA, YAFUZU KIBABE CAF

Written by mzalendoeditor

 

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufanikiwa kuichapa Horoya AC kwa mabao 7-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa.

Simba Sc ilianza kupata bao kupitia kwa Clatous Chama ambaye alipiga mpira wa adhabu  na kutinga moja kwa moja wavuni  na baadae Jean Baleke akapachika  bao  la pili baada ya Kipa wa Horoya kuokoa shuti kali  lililopigwa na Kibu Denis na kukuta Baleke na kuzamisha wavuni.

Bao la tatu limefungwa kwa njia ya penati kupitia kwa nyota wao Chama ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Horoya kuunawa mpira na kuamlishwa penati.

Mpaka mapumziko  Simba Sc ilikuwa iko mbele kwa mabao 3-0, huku kipindi cha pili wakirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata mabao mengine kupitia kwa Baleke na kufiikisha  mabao mawili  kwenye mchezo huu, Chama ambaye amefunga matatu (Hat Trick) pamoja na Sadio Kanoute ambaye nae amefunga mawili

About the author

mzalendoeditor