Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Wizara itaendeleza misingi iliyoachwa na viongozi waliotangulia katika Wizara hiyo ili kuwezesha kutimiza malengo yake. 
 
Prof. Nombo amesema hayo Machi 13, 2023 jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Francis Michael ambapo amesema nyaraka alizokabidhiwa kwake ni nyenzo muhimu kwa ajili ya uendelezaji wa kazi za Wizara.
 
Katibu Mkuu huyo amemshukuru Dkt. Michael kwa kumlea wakati akiwa Naibu Katibu Mkuu  kwani kupitia yeye amejifunza mengi. Aidha amemuomba kuwa balozi wa sekta ya Elimu Sayansi na Teknolojia katika Mkoa wa Songwe ambako kwasasa ni Mkuu wa Mkoa huo.
 
Naye Dkt Francis Michael amempongeza Katibu Mkuu Nombo kwa kuaminiwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba yupo tayari kutoa ushirikiano na ushauri wowote atakapoitajika kufanya hivyo.

Previous articleWANAFUNZI WA KIKE 96 WA SHULE ZA SEKONDARI KUPATIWA MAFUNZO YA TEHAMA DIT
Next articlePOLISI YAELEZA CHANZO CHA KIFO CHA MCHIMBAJI MADINI KINYUME NA UTARATIBU NORTH MARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here