Featured Kitaifa

NEMC YAWEKA WAZI MAFANIKIO YAKE KATIKA KIPINDI CHA AWAMU YA SITA

Written by mzalendoeditor

 

MKURUGENZI Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) , Dkt. Samwel Gwamaka, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Machi 3,2023 jijini Dodoma wakati akielezea mafanikio ya Baraza hilo  katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita.

 

SEHEMU ya Waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) , Dkt. Samwel Gwamaka, wakati akielezea mafanikio ya Baraza hilo  katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 3,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limesema katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 wamesajili jumla ya miradi takribani 1,702 ikiwemo ya tathimini ya athari za mazingira na ya ukaguzi wa mazingira.

Hayo yameelezwa leo Machi 3,2023 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa NEMC Dk Samweli Gwamaka,wakati akielezea  mafanikio ya Baraza hilo katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa serikali ya awamu ya sita.

“Kwa kupitia taarifa za tathimini ya athari kwa Mazingira katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 Baraza limefanikiwa kusajili miradi takribani 1702, ambapo kati yake 967 ni ya (TAM) na 735 ni ya ukaguzi wa mazingira.

“Aidha baraza liko katika hatua za mwisho kwa ajili ya kuanazisha kanda nyingine nne ili kuendelea kusogeza huduma karfibu zaidi ya wananchi”amesema  Dk. Gwamaka.

Hata hivyo Dk.Gwamaka,amesema katika  kipindi cha mwezi Julai 2021 hadi Februari 2022,NEMC imepokea  na kushughulikia malalamiko takribani 369 ya uchafunzi na uharibifu wa mazingira kutoka kwa wannachi.

Amesema  malalamiko hayo ni pamoja na kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye mabomba ya mafuta, kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango kinachotakiwa kisheria, uchafusi wa vyanzo vya maji, uturirishaji wa maji taka, uchafunzi wa hewa kutokana na shughuli za viwanda.

“Malalamiko mengine ni pamoja na kelele za muziki,kushamiri kwa gereji bubu maeneo ya makazi,kushamiri kwa vituo vya mafuta katikati ya makazi,matumizi ya mifuko ya plastiki iliyokatwazwa na kutapakaa maeneo ya makazi na kuhakikisha inatoa elimu juu ya jambo husika”amesema Dk. Gwamaka

Pia, amesema  katika kipindi hicho Baraza limekuwa likishughulika na udhibiti wa taka ngumu kama vile utekelezaji na utoaji wa vibali ambapo uteketezaji wa taka hatarishi kama dawa na bidhaa za viwandani zilizokwisha muda wake umefanyika.

“Aidha, kushughulikia maombi ya vibali vya taka hatarishi aina ya chuma chakavu,betri chakavu,taka za kielektroniki,tairi chakavu,taka za kemikali na taka za plasitiki ikiwa ni pamoja na maombi ya vibali vya kuingiza au kupitisha nchini pamoja na kusafirisha nje ya nchi”amesema 

Amesema  pia Baraza limefanikiwa kuanazisha Kanda tisa nchini nzima zenye wataalamu wa mazingira wanaotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 wakishirikiana na wadau, halamashauri za miji na wilaya hali iliyorahisisha utatuzi wa kero za kimazingira.

Amesema kuwa  Baraza limetoa jumla ya vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya nchi,vibali 10 vya kuingiza au kupitisha na kusafirisha nje ya nchina kupeleka kiasai cha tani 516,041 za taka mbalimbali zilizokusanywa na makampuni yenye vibali hali inayoonesha uwajibikaji katika kuhakikisha sheria ya mazingira inayozingatia uhifadhi na utunzaji wake inazingatiwa.

Aidha ameeleza kuwa Baraza hilo limepanga kuanzisha klabu za utunzaji wa mazingira kuanzia  ngazi ya shule za msingi na sekondari ili kuwajengea watoto  msingi mzuri wa namna ya kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yao.

Amesema NEMC inaanzisha klabu za mazingira na kuzilea  kwa sababu watoto  wakianza kufundishwa wakiwa katika umri mdogo ni rahisi zaidi kuelewa umuhimu wakutunza mazingira na faida zake kijamii,kiuchumi na kiafya.
“Sasa tunajikita  kuelimisha na kukikamata kizazi cha watoto wadogo kuanzisha shule za msingi na sekondari ili wachukulie suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu lao la kila siku katika mwenendo mzima wa maisha yao.Tunaamini watakapo kuwa wakubwa tabia itakuwa imejengeka ,”amesema Dk.Gwamaka

About the author

mzalendoeditor