Featured Michezo

SIMBA SC YATINGA ROBO FAINALI ASFC KIBABE

Written by mzalendoeditor
TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Africans Sports ya Tanga mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Jean Baleke dakika ya 36, beki Kennedy Juma dakika ya 47, mshambuliaji Mzanzibari Mohamed Mussa dakika ya 69 na beki Jimmyson Mwanuke dakika ya 90.

About the author

mzalendoeditor