Featured Kitaifa

BRELA YAKUTANA NA WATAALAMU WA  VYOMBO VYA UCHUNGUZI JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

MKURUGENZI wa Idara ya Kampuni na Majina ya Biashara kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.Meinrad Rweyemamu,akizungumza wakati wa kikao cha majalidiliano kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa baina ya wakala na vyombo vya uchunguzi  leo Machi 2,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA ,Godfrey Nyaisa.

KAIMU Kamishna wa Uhamiaji,Charles Kasambula,akielezea umuhimu wa mafunzo hayo wakati wa kikao cha majalidiliano kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa baina ya wakala na vyombo vya uchunguzi  leo Machi 2,2023 jijini Dodoma.

MKURUGENZI wa Idara ya Kampuni na Majina ya Biashara kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.Meinrad Rweyemamu,akitoa mada kwa washiriki wa mafunzo wakati wa kikao cha majalidiliano kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa baina ya wakala na vyombo vya uchunguzi  leo Machi 2,2023 jijini Dodoma.

 

MKURUGENZI wa Idara ya Kampuni na Majina ya Biashara kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw.Meinrad Rweyemamu,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua  kikao cha majalidiliano kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa baina ya wakala na vyombo vya uchunguzi  leo Machi 2,2023 jijini Dodoma kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA ,Godfrey Nyaisa.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAKALA ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewataka wataalamu wa vyombo vya uchunguzi kuhakikisha wanafanikisha mkataba wa taifa wa kudhibiti na kupambana na utakatishaji wa fedha haramu.

Hayo yameelezwa leo  Machi 2,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Kampuni na Majina ya Biashara kutoka BRELA,Meinrad Rweyemamu wakati wa kikao cha majalidiliano kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa baina ya wakala na vyombo vya uchunguzi  kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA ,Godfrey Nyaisa.

Rweyemamu amewataka  wataalamu hao  kuhakikisha wanafanikisha mkataba wa taifa wa kudhibiti na kupambana na utakatishaji wa fedha haramu.

“Wakala ilitoa access ya mifumo yetu ya ndani ikiwemo mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao na mfumo wa wamiliki manufaa kwa vyombo vya uchunguzi,”amesema Rweyemamu

Aidha Rweyemamu,amesema BRELA  imekuwa ikishirikiana kwenye shughuli mbalimbali za kiutendaji ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho mbalimbali ya kisheria na kimfumo ili kuhakikisha wanatoa   huduma bora.

Amesema makampuni yana umuhimu mkubwa katika kuchangia uchumi wa Nchi hata hivyo uzoefu umeonesha kuna baadhi yanatumika vibaya kama kufanya vitendo vya kiuhalifu visivyokubalika katika jamii.

“Ikiwa ni pamoja na utakatishaji wa fedha haramu,kufadhili vitendo vya kigaidi pamoja na vitendo vya rushwa na hata ukwepaji wa kodi,”amesema

Amesema Benki ya Dunia na taasisi zingine zimejitolea kuleta mabadiliko ya hali hiyo kwa kuanzisha dhana ya wamiliki manufaa ambayo imeungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.

Amesema kwa kuwezesha juhudi hizo Taasisi ya Kimataifa ya Financial Action Task Force (FATF) mwaka 2014 ilitoa muongozo kwa taasisi ya Kimataifa ya Globar forum on Transparency and Exchange of Information for Tax Purposes.

“Juu ya jinsi ya kuyashughulikia masuala ya ukusanyaji wa taarifa za wamiliki manufaa ya makampuni,”amesema 

Kwa upande wake,Kaimu Kamishna wa Uhamiaji,Charles Kasambula amesema mafunzo hayo ni muhimu kutokana na dunia ilivyo kwenye suala zima la utakatishaji fedha.

“Tukiwa kama nchi ni vyema tukapata mafunzo haya na sisi kama wahamiaji wawekezaji lazima wapite kwetu ili kuweza kupata vibali vya kuishi na kuwa na makazi nchini,hivyo itasaidia watu wanapoanzisha kampuni zao hasa wa nje kuweza kuchunguza vyanzo vya pesa zao ili tuwe na watu safi sio watu wanaotaka kutakatisha pesa zao,”.

About the author

mzalendoeditor