Featured Kitaifa

NDEJEMBI,NDUNGURU NA MTWALE WAANZA KAZI TAMISEMI WAPOKELEWA KWA SHANGWE

Written by mzalendoeditor

 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius J. Ndejembi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Adolf H. Ndunguru na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Sospeter M. Mtwale wameripoti Ofisi za Wizara zilipo Mji wa Kiserikali Mtumba na kupokelewa na Menejimenti na baadhi wa Watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Leo tarehe 28 Februari,2023.

Hafla hiyo ya mapokezi imefanyika Ofisi ya Rais TAMISEMI Mji wa Serikali Mtumba na kufuatiwa na kikao cha menejimenti ambapo kitaingozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius J. Ndejembi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI , Mhe. Angellah Kairuki katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba – Dodoma, leo tarehe 28 Februari, 2023.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Adolf H. Ndunguru akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI , Mhe. Angellah Kairuki katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba – Dodoma, leo tarehe 28 Februari, 2023.

  

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Sospeter M. Mtwale akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI , Mhe. Angellah Kairuki katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba – Dodoma, leo tarehe 28 Februari, 2023.

About the author

mzalendoeditor