Featured Kitaifa

DC MWEMA AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VYANDARUA KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI CHAMWINO

Written by mzalendoeditor

MKUU wa Wilaya ya  Kongwa ,Remidius Mwema,akiwakabidhi baadhi ya Wanafunzi Vyandarau  wakati wa hafla ya zoezi la upokeaji na ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi za wilaya ya  Chamwino hafla  iliyofanyika leo Februari 28,2023 katika Shule ya Msingi Buigiri Misheni wakati akimwakilisha  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,Gift Msuya.Kulia ni Meneja wa Kanda Bohari ya Dawa (MSD) Dodoma,John Sipendi.

MKUU wa Wilaya ya  Kongwa ,Remidius Mwema,akizungumza  wakati wa hafla ya zoezi la upokeaji na ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi za wilaya ya  Chamwino hafla  iliyofanyika leo Februari 28,2023 katika Shule ya Msingi Buigiri Misheni wakati akimwakilisha  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,Gift Msuya,

MENEJA wa Kanda Bohari ya Dawa (MSD) Dodoma,John Sipendi,akielezea mpango wa kusambaza Vyandaru katika Mkoa wa Dodoma wakati wa  zoezi la upokeaji na ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi za wilaya ya  Chamwino  hafla iliyofanyika leo Februari 28,2023 katika Shule ya Msingi Buigiri Misheni.

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Buigiri Misheni wakifatilia hafla ya upokeaji na ugawaji wa Vyandarau.

AFISA Elimu Msingi Wilaya ya Chamwino Bi.Zaina Kishegwe,akizungumza wakati wa  zoezi la upokeaji na ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi za wilaya ya  Chamwino  hafla iliyofanyika leo Februari 28,2023 katika Shule ya Msingi Buigiri Misheni.

KAIMU Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Dk.Venance Mgaiga,akizungumza wakati wa  zoezi la upokeaji na ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi za wilaya ya  Chamwino  hafla iliyofanyika leo Februari 28,2023 katika Shule ya Msingi Buigiri Misheni.

MKUU wa Wilaya ya  Kongwa ,Remidius Mwema,akiwakabidhi baadhi ya Wanafunzi Vyandarau  wakati wa hafla ya zoezi la upokeaji na ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi za wilaya ya  Chamwino hafla  iliyofanyika leo Februari 28,2023 katika Shule ya Msingi Buigiri Misheni wakati akimwakilisha  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,Gift Msuya.Kulia ni Meneja wa Kanda Bohari ya Dawa (MSD) Dodoma,John Sipendi,

MKUU wa Shule ya Msingi Buigiri Misheni Nassib Khatibu,akitoa neno la shukrani mara baada ya uzinduzi wa zoezi la upokeaji na ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi za wilaya ya  Chamwino hafla  iliyofanyika leo Februari 28,2023 katika Shule ya Msingi Buigiri Misheni .

MKUU wa Wilaya ya  Kongwa ,Remidius Mwema,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mara baada ya kuzindua  zoezi la upokeaji na ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi za wilaya ya  Chamwino hafla  iliyofanyika leo Februari 28,2023 katika Shule ya Msingi Buigiri Misheni wakati akimwakilisha  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,Gift Msuya.

 

Na.Alex Sonna-CHAMWINO

SERIKALI imezindua zoezi la ugawaji vyandarua vilivyowekewa dawa kwa wanafunzi wa shule za msingi za Serikali na Binafsi lengo likiwa ni kuhakikisha wanakabiliana na changamoto ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkuu  wa Wilaya ya  Kongwa ,Remidius Mwema,akizungumza  wakati wa hafla ya zoezi la upokeaji na ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi za wilaya ya  Chamwino hafla  iliyofanyika katika Shule ya Msingi Buigiri Misheni akimwakilisha  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino,Gift Msuya.

DC Mwema amewataka viongozi wanaohusika na zoezi hilo kusimamia kikamilifu  ugawaji wa vyandarua hivyo ili viweze kuwafikia walengwa na si watu wengine.

“Nitoe wito viongozi kusimamia zoezi hili ili liweze kuleta tija katika Wilaya yetu ya Chamwino”amesema Mwema.

Amesema shule ya Buigiri Misheni ina bahati kubwa katika shule 127 zilizopo wilayani humo kwa kuchaguliwa kuwa sehemu ya uzinduzi huo.

Amesema zoezi hilo lengo lake ni kuwalinda wanafunzi dhidi ya ugonjwa wa malaria na kutimiza kwa vitendo dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya angalau kila mwanafunzi mmoja aweze kupata chandarua chake.

“Vyandarua hivi vinawalenga nyinyi wenyewe nataka nitume ujumbe kwenu usije ukachukua chandarua ukaenda nyumbani ukaenda kumpa mzazi kwamba  tumepewa tukuletee.

“Ninafahamu  yamekuwa  matumizi mengine mnaenda kutumia kulimia mchicha au bustani nataka niseme hapana,nasema hapana sio matumizi sahihi semeni hapana,”amesema Mwema

Amesema Serikali inawapenda na nia yake ni kuhakikisha wanakuwa na afya njema.

Hata hivyo amewataka wanafunzi hao kuvitumia kwa matumizi sahihi mara baada ya kumaliza kusoma.

“Tunahitaji watoto wetu muwe na afya njema,ukiwa na afya njema utaweza kutimiza ndoto zako.Serikali inawapenda ndio maana jitihada zimechukuliwa,”amesema 

Aidha amesema wanahitaji kila mwanafunzi aweze kutambua umuhimu wa kutunza afya.

“Nendani mkawaambie wazazi wenu,majirani kwamba vyandarua hivi haviuzi na yoyote atakaeuza atachukuliwa hatua kali za kisheria,imani yangu mnaenda kufanya matumizi sahihi.

Amesema mpaka sasa Wilaya hiyo imepokea vyandarua 17556 kwa wanafunzi zaidi ya 88,000.

Amesema wataendelea kuhimiza viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na viongozi wa kisiasa.

“Niwaombe mtusaidie pale ambapo mtabaini anapotosha lengo msisite kutoa taarifa ili muweze kutusaidia wengine watakuwa matumizi mengine kwenye kuvua samaki,hayo mambo hatutaki.

“Tutaendelea kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara,katikati ya Machi tutafanya ufuatiliaji wenu kwa kila mmoja,”amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

Kwa upande wake Meneja Kanda Bohari ya Dawa (MSD) Dodoma,John Sipendi, amesema wamezindua usambazaji wa vyandarua katika shule za wilaya ya Chamwino.

Amesema zoezi hilo linaratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( Tamisemi).

Amesema Kwa Mkoa wa Dodoma wanatarajia kusambaza zaidi ya vyandarua 560,000 ambavyo watazifikia shule 862.

“Niwatake wanafunzi waendelee kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa lengo  ni kuzuia maambukizi yaweze kufikia asilimia 0 kwani kwa Wilaya ya Chamwino kuna maambukizi asilimia 0.7,”amesema Bw.Sipendi

Naye,Mkuu wa Shule ya Buigiri Misheni,Nassibu= Khatibu amesema watatoa elimu kwa wanafunzi ili watumie vizuri vyandarua hivyo.

“Tutawaelekeza Wazazi na walezi kwa kuwa tuna mikutano tutaelekeza jinsi ya kuvitumia vizuri,”amesema.

About the author

mzalendoeditor